Monday, July 28, 2014

NELSON PAMOJA NA DADA YAKE SARA UWERA WAKIIMBA KWA HISIA WAKATI WA KUREKODI.

YUSTO AKIIMBA.

FLORA PAMOJA NA PEPE WAKIIMBA KWA FURAHA

JIMMY MMOJA KATI YA SOLO WA MDA MREFU AKIPAZA SAUTI YAKE KUMPA SIFA MUNGU

JOSEPH NAE HAKUWA NYUMA KUMTUKUZA MUUMBA WAKE


KJ MARCELLO AKIIMBA KWA TABASAMU KUBWA NA NDIYE MMILIKI WA PICHA ZOTE.


HAPA WAKIIMBA

PICHA YA PAMOJA BAADA YA HUDUMA

Kwa mara nyingine kwaya ya Ambassadors of Christ ya nchini Rwanda siku ya jumanne wiki iliyopita ilirekodi dvd yake live huko Kigali nchini Rwanda ikipewa jina la 'Ibatebuli recording concert' na kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi wa kwaya hiyo ambayo walivaa sare zao nadhifu na zenye kupendeza.
Tukio hilo la kurekodi ambalo jina lake 'Ibatebuli' ni lugha ya Tonga inayozungumzwa nchini Zambia na Malawi linamaanisha wavunaji ikiwa ni tafsiri ya wimbo wao maarufu wa 'Abasaruzi' ambao kwasasa pia umetafsiriwa kwa lugha hiyo ya Tonga ikiwa ni kupanua wigo zaidi wa injili kwa kwaya hiyo ambayo ilipokelewa kwa kishindo nchini Zambia mwishoni mwa mwaka jana ilipokwenda kutoa huduma licha ya kwamba Zambia ina kwaya zenye nguvu na uimbaji maridadi.
Kwaya hiyo ambayo imekuwa ikitoa album zake kwa lugha ya kwao kinyarwanda pamoja na kiganda huzitafsiri nyimbo zao kwa lugha ya kiswahili pia jambo ambalo si tu linaongeza wigo wa uinjilishaji lakini pia mapato ya kwaya hiyo yanaongezeka na kuwawezesha kusonga mbele na huduma yao. Ambapo kwasasa wameanza mikakati ya kuimba lugha nyingi zaidi ikiwemo hiyo ya Tonga ili kuwafikia watu wengi zaidi ili wamjue Mungu.

habari kwa hisani ya http://www.gospelkitaa.co.tz
















*** TUMA PICHA NA HABARI KWA WATSUP SASA NO 0717-367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA