Saturday, November 29, 2014

Utambulisho huu ulifanywa katika siku ya uwekaji wakfu wa kanisa la Kimara Sda na mchunagaji wa mtaa Rahis Mande ambaye ndiye mwenyeji alifanya utambulisho huu akianzia wazee wa kanisa la Kimara na baadae wageni waalikwa na wawakili toka makanisa yaliyoalikwa siku hiyo na mgeni rasmi kwa siku hiyo alikuwa ni Sadock Butoke katibu mkuu wa jimbo la mshariki mwa Tanzania..
Mchungaji wa mtaa wa Kimara Rahisi Mande akitambulisha wazee wa kanisa na wageni wa siku hiyo.
Mchungaji Toto Kusaga akizungumza mara baada ya kutambulishwa na baadae akawa na muda wa kutoa somo katika maandiko matakatifu.
Mzee wa kwanza wa kanisa la Kimara,Yusuph Azizi naye akisimama mara baada ya kutambulishwa na mchungaji wa mtaa wa kimara..
Moja kati ya wazee wa kanisa wa sasa,Mzee Kilimo nae akitambulishwa siku hiyo..
Mzee Joshua Manyama mshiriki na aliyewahi kuwa mzee wa kanisa la Kmiara akipungia washiriki mikono mara baada ya kutambulishwa siki hiyo..
Kulia ni mchungaji aliyemaliza mda wake kwa nafasi ya mchungaji wa mtaa katika kanisa la Kimara Mchungaji Mbuti Kusekwa na kushoto ni mchungaji wa sasa mtaa wa Kimara mchungaji Rahisi Mande akitoa utambulisho huo..
Mchungaji Buluma akisema neno mara baada ya kutambulishwa siku maalum ya kuwekwa kwa kanisa la Kimara.
Mzee Sekiete mshiriki wa Kanisa la Kimara sda nae akitambulishwa siku hii.
Mzee Msese toka kanisa la waadventista wasabato Suka akipunga mkono mara ya kutambulishwa..
Mchungaji Steven Letta akisema maneno machache mara baada ya kutambulishwa.

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA