Wednesday, January 28, 2015


Simulizi hizi muhimu zitakuwa zinakujia kwa siku 3 yaani Jumatano,ijumaa na jumapili.                             
        Imeandaliwa na Mch J.Kuyenga
                Historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato katika sehemu za     kati,Mashariki,Kusini na magharibi mwa Tanzania.
 Mwanzo wa utume jijini Dar Es Salaam
Mwaka 1958 wainjilisti wa vitabu,Ndugu Misheto na Ndugu Bariki Mgeni waliingia mjini Dar Es Salaam.Mchungaji Fares Muganda alifanya mahubiri kule Amana Hall mwaka huo 1958,wakaongolewa watu 21 kama vile,Musa bin Musa,Nanga Munji,Hakimu na wengine wengi wakahamishiwa katika kanisa la Magomeni lililofunguliwa mara baada ya mahubiri ya Pr.E.E.Cleverland mwaka 1963.
Kanisa la Mungu likachukua sura mpya kabisa katika mji wa Dar Es Salaam kutokana na mahubiri ya Pr.E.E.Cleverland 1963 washiriki kiasi cha 75 walibatizwa na wakawa wanakutanika katika kanisa la Magomeni kutoka kila sehemu ya mji kila Sabato kwa ibada.Pr Bender na Pr.Kuyenga walikuwa na kazi ngumu ya kuwatafuta waumini hawa wapya waliotawanyika katika mji mzima wa wakati huo.Pr.Kuyenga asema"Hapa tulikutanika watu wa mataifa mengi maana mahubiri haya yalileta watu katika mji kutoka idara mbalimbali za serikali na sababu ya utaratibu mzuri kanisani na kwa nyimbo za kwaya,ongezea mwonekano wa jengo,tulikutanika kwaribu washiriki wote kila Sabato.Wafanyakazi kama vile;Mwinjilisti Misheto,Pr.Kusekwa,Pr.G.Mbwana waliwahi kuishi katika nyumba za Magomeni wakiwa waongozi wa idara ya vitabu kutoka Union"
Mji wa Morogoro
Cheche za injili katika mji wa Morogoro ziliingizwa na Mwinjilisti Yohana Lukwaro tangu mwaka 1958.Akiwa yeye na mtoto mmoja walikaribishwa na mzee Kucharsk aliyekuwa mkulima wa misufi(Kapok) katika eneo lote la uwanja wa makao makuu ya Konferensi na T.A.P kwa sasa.Wakati huo eneo hili lilikuwa kama msitu wa misufi likiwa na nyumba moja tu ambayo ipo hata leo ilitumiwa na huyu mzee na mke wake,iliyo karibu sana na jengo la ofisi za Fildi.Hapo ndipo mzee Lukwaro na familia yake walipoanza kukutana kwa ibada kila sabato.Familia hii inakumbuka ukaribu wa mzee huyu wa kiadventista Msabato hasa kutuma kijana wake kuja kuwapokea kutoka station ya treni.

INAENDELEA JUMATANO......
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA