NAIROBI:THE LIGHTBEARERS WAREKODI NYIMBO KATIKA STUDIO ZA HOPE CHANNEL AFRICA
Copy the BEST Traders and Make Money (One Click) : http://ow.ly/KNIC
Copy the BEST Traders and Make Money (One Click) : http://ow.ly/KNIC
Jumla
ya Waimbaji 19 wa The LightBearers wako jijini Nairobi,Kenya kwa ziara maalum
ya uimbaji ambapo watashiriki kwenye Tamasha la Uimbaji litalofanyika leo
jumapili Agosti 30,mwaka kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni kwenye
ukumbi wa Nairobi Cinema. Jana Agosti 29 jioni walikuwa katika studio za Hope
Channel Africa zilizopo yalipo Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato
Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD) eneo la Ongata Rongai ambapo
wamerekodi nyimbo tano za video ambazo zitarushwa na kituo hicho cha
Televisheni kinachorusha matangazo yake kupitia satalaiti kwa kushirikiana na
Hope Channel International.
--------------------------------
Baada ya Tamasha la leo The LightBearers
wataelekea jijini Arusha kisha Mwanza ambako watashiriki kwenye tamasha
litakaloambatana na kuitambulisha album yao namba 3 iitwayo MUNGU kimbilio
tukio litakalofanyika kwenye ukumbi wa Vijana Mlango Mmoja Septemba 5 mwaka huu
saa nane mchana.
Picha/Habari na Mtangazaji Blog
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment