Monday, April 11, 2016

1 Wakorintho 6:18 "Ikimbieni ZINAA. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe".
Kati ya mishale yenye sumu anayotumia mkuu wa Giza "aka" Shetani kujeruhi na kuua wengi ni ZINAA na UASHERATI. Hili limekuwa janga la kimataifa, bila kujali una Dini au Laa.
Wengi wametengwa na Uso wa Bwana kwa kunaswa na mtego huu wenye sumu, unaopofusha macho na masikio ya Kiroho. Waimbaji na hata wahubiri wa Injili wanaweza kuimba "Usizini", "Acha dhambi", "Tumeokolewa", "Tuko ndani ya Yesu " n.k. Huku ni wazinifu ingawa ni kwa siri, hao wote ni Marehemu wanaotembea.
NENO la leo linasema IKIMBIENI ZINAA, Wengi wamejikuta wamejeruhiwa bila kutarajia kwa sababu ya kuruhusu mjadala na Shetani, zinaa inakimbiwa, haijadiliwi. Mazingira yote ya faragha kwa watu wawili walio jinsia tofauti ni hatari, Wengi ni mashahidi, na wengi yamewakuta.
Wito: Ni wakati wa kuvaa SILAHA zote za Mungu kwa njia ya Roho mtakatifu. Ni nani Yusufu wa leo? Kwa nini usiwe wewe?. Wapendwa msidanganyike hakuna faida kwenye maisha ya Dhambi, ni HASARA TU NA VILIO NA KUDHARAULIWA.
NAWATAKIA MAPUMZIKO MEMA.
Na. Ev. Eliezer Mwangosi. ...

 ****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA