Showing posts with label LESONI. Show all posts
Showing posts with label LESONI. Show all posts

Sunday, June 19, 2022

 Soma Mwanzo 46. Kuondoka kwa Yakobo Kanaani kuna umuhimu gani?

 

Yakobo anapoondoka kwake Kanaani, amejawa tumaini. Uhakikisho kwamba hataona njaa tena, na habari njema kwamba Yusufu yu hai, ni lazima vilimpa msukumo kwamba anapaswa kondoka katika Nchi ya Ahadi.

Kuondoka kwa Yakobo kunatoa mwangwi wa uzoefu wa Ibrahimu, ingawa kwa habari ya Ibrahimu alikuwa anaelekea katika Nchi ya Ahadi. Yakobo anasikia ahadi ile ile ya Ibrahimu ambayo Ibrahimu aliisikia toka kwa Mungu, yaani kwamba atamfanya kuwa “taifa kubwa” (Mwa. 46:3; linganisha na Mwa. 12:2). Wito wa Mungu hapa pia ni ukumbusho wa agano la Mungu na Ibrahimu; katika matukio yote Mungu anatumia neno lile lile linalotoa uthibitisho tena “ ‘usiogope’ ” (Mwa. 46:3; linganisha na Mwa. 15:1), linalobeba ahadi ya maisha yajayo yenye utukufu.

Kuorodheshwa kwa upana kwa majina ya watoto wa Israeli walioenda Misri, pamoja na binti zake (Mwa. 46:7), kunakumbusha ahadi ya Mungu ya uzao mwingi kwa Ibrahimu hata wakati akiwa bado hana mtoto. Namba “sabini” (pamoja na Yakobo, Yusufu, na wanawe wawili) inaelezea wazo la utimilifu/ukamilifu. Ni “Israeli yote” inayokwenda Misri. Ni muhimu pia kwamba namba 70 inafanana na namba ya mataifa (Mwanzo 10), kuashiria kwamba hatima ya mataifa yote ina hatarishwa katika safari ya Yakobo.

Ukweli huu utakuwa dhahiri zaidi tu miaka mingi baadaye, baada ya msalaba na ufunuo kamili zaidi wa mpango wa wokovu, ambao, bila shaka, ulikuwa kwa ajili ya wanadamu wote, po pote, na si tu kwa watoto wa Ibrahimu.

Kwa maneno mengine, hata kama visa vinavyohusu familia hii vinavutia, uzao wa Ibrahimu, na masomo yo yote ya kiroho tunayoweza kujifunza kutokana nayo—simulizi hizi ziko katika neno la Mungu kwa sababu ni sehemu ya historia ya wokovu; ni sehemu ya mpango wa Mungu wa kuleta ukombozi kwa watu wengi iwezekanavyo katika sayari iliyoanguka.

“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, ‘Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka’ ” (Rum. 10:12, 13). Paulo anasema nini hapa kinachoonesha kuwa injili ni kwa ajili ya ulimwengu wote? Muhimu zaidi, maneno haya yanatuambia nini kuhusiana na kile ambacho sisi kama kanisa tunapaswa kufanya ili kusaidia kuitangaza injili?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Wednesday, August 31, 2016

Makanisa ni makundi yanayojitolea kwa sehemu kubwa, yanayofanya kazi katika bajeti finyu.Mtaji wa kijamii husaidia husaidia makanisa mahaliakuongeza nafasi ya kuyafikia malengo yake muhimu. Utamaduni wa kale katika baadhi ya nchi huwasaidia wakulima wengine kuleta mavuno yao ni mfano wa mtaji wa kijamii. Hii ni kwamba ingawa inatupasa kuangalia kila hali kwa jinsi yake, lakini pale inapowezekana ni busara kufanya hivyo, tunaweza kushirikiana na wengine ilikuyafikia malengo yetu.

Soma Nehemia 2:1-9.Ni nini iliyokuwa matokeo ya matumani kutoka mbinguni aliyokuwa nayo mfalme Artashasta juu ya Nehemia?
Fedha ambazo alikuwa amepungukiwa (Nehemia) aliomba kwa wenye uwezo wakampatia. Bado Bwana yupo tayari kugusa mioyo ya wale wanao miliki maliza zake kwasababu ya kuendeleza njia ya ukweli. Wale wanaomtumikia Bwana katika kazi zake wanapaswa kupokea msaada ambao anawasukuma watu wake kutoa…Wenye kutoa misaada wanaweza wasiwe na Imani kwa Kristo wala kufahamu maneno yake; lakini michango yao isikataliwe kwasababu hiyo. “Ellen G.White, Prophets and Kings, uk.634.

Huvutia kiasi gani kwamba katika jambo hili Mungu aligusa mioyo ya wapagani ili kuendeleza kazi yake.Hili linapaswa kutufundisha jambo la muhimu sana hapa. Kwa viwango vyovyote vile tunavyoweza kufikia ni lazima tuwe tayarin kufanya kazi pamoja na watu wengine,hata wale wasio na Imani yetu au wasio na Imani kabisa, Kama kwa kufanya hivyo tutaiendeleza kazi ya Kristo kusonga mbele Zaidi. Ingawa kwa hakika tunapaswa kuwa makini katika ushirikiano tunaouanzisha na watu wengine. Kwa uangalifu na kwa njia ya maombi mengi tunaweza kuifanya kazi na wengine ambao michango yao yaweza kuisaidia kazi ile tunayo hitaji kuifanya kwa ajili ya ustawi wa jumuiya yote. Mara kadhaa serikali, hata mashirika binafsi na wafanyabiashara binafsi, wanapovutia na kazi zetu za kujali wengine, watatupatia msaada wao, Msaada huu haupaswi kukataliwa moja kwa moja au kukubaliwa moja kwa moja bila kufikiri. Badala yake, utazamwe kwa maombi na misingi ya vipengele tofauti tofauti, na kwa nyenzo mbali mbali na ushauri wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi.
Ni njia zipi unazoweza kujenga “mtaji wa kijamii”katika jamii yako ambao waweza kuleta matokeo chanya, bali sio mafanikio yako bali mafanikio kwa wengine?
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, August 30, 2016

“Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; na neema kuliko fedha na dhahabu.” (Mithali 22:1). Ni kwajinsi gani dhana inayo oneshwa hapa inahusiana na jinsi tunavyo shuhudia na kuwafikia wengine? 

Nini “maana ya mtaji wa kijamii” wakati unapo wekeza katika akaunti ya benki thamani yake hukua. Mtaji wa kijamii hujumuisha uhusiano chanya na wenye faida kama pesa katika benki. Wakati unapo jenga maelewano mazuri na viongozi wa jamii, waulize ni nini yalio mahitaji ya jamii, tafuta ushauri kwao kwamba nini kifanyike kutatua matatizo hayo,Ikifuatiwa na utekelezaji wa mahitaji hayo,Kwa kufanya hivyo utakuwa unajenga na kukuza uhusiano mzuri nao.Huu ni mtaji wa kijamii, kila uzoefu chanya unao jenga pamoja nao ni kama uwekezaji katika uhusiano wenu, Mtaji wako wa kijamii huendelea kukua na kuongezeka thamani machoni pao.

Kanuni ya Kanisa hutukumbusha kwamba Waadventista Wasabato,”tunapaswa kutambuliwa kama raia wema…na kufanya mambo yaliyo mema”. “tunapaswa kuisaidia jamii kwa kutoa huduma zetu na vipato vyetu,kwa kadri inavyowezekana na kwa kufuatana na Imani zetu, nguvu zetu kwa ajili ya kudumisha utulivu wa kijamii na ustawi wake,” Huku tukidumisha misimamo thabiti ya haki na kweli katika mambo ya kijamii,”- Standard of Christian Living,” Uk.137,138.in the Seventh day Adventist Church Manual.( Hagerstown,Md.:Review and Herald Publishing Association,2010)
Katika nyongeza ya huduma ya Yesu duniani, maandiko hutupa mifano mingine ya kile ambacho kinaweza kutokea ikiwa watu wa Mungu watakuwa wamejipatia, “mtaji wa kijamii” Soma vifungu vifuatavyo vya maneno na ueleze uhusiano chanya ambao wahusika hawa katika Biblia walipata uzoefu wa kuwa pamoja na “watu wa nje” na ni nini kilichotokea kama matokeo? Matendo 7:9,10, Wagalatia 41:38-45,Danieli 2:46; 6: 1-3.

Kwa hakika,tusiwe na aina hii yay a visa vyenye mvuto kama hivi vilivyoonekana hapa.Lakini hiyo siyo hoja ya msingi, hawa watu walionesha uuthabiti wa tabia iliyo wavutia waliokuwa wamewazunguka-Ellen G.White alizungumza katika kitabu cha Patriarchs and Prophets uk.217,218,221 na katika Prophets and Kings, uk. 628 Anaelezea kwamb katika sifa walizokuwa nazo watu hawa wa Mungu ziliwafanya watu hawa waaminiwe na kupendwa na “wapagani”walio kuwa karibu nao ni :Upole.uaminifu, hekima, maamuzi mema, matajiri, tabia njema na uadilifu thabiti.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Monday, August 29, 2016

Kanisa mojawapo la waadventista wasabato katika nchi za Afrika linakua kwa kasi. Nini siri yao? Viongozi wa kanisa walisema kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya ukuaji huu na kutokua ubinafsi na huduma zisizo na masharti za washiriki wa kanisa lile kwa jamii inayo wazunguka na taifa kwa ujumla. Kujiamini kwa kanisa hili kuliko enea nchi nzima kulichukua umakini wa rais wanchi hiyo. Alihudhuria mkutano mkubwa wa hadhara ulioendeshwa na kanisa hilo la waadventista wasabato aliwashukuru washiriki wakanisa lile kila mmoja kwa huduma yake.

Wakati huo huo kama wawakilishi wa Kristo tunapaswa kutembea katika njia nyembamba. Tunahitajika, kama Yesu alivyo fanya, kuishinda Imani na kujiamini kwao. Lakini Imani na rtumaini lao kwetu linapaswa kupelekwa moja kwamoja kwa Kristo. Sisi ni mifereji tu. Wanamwona Kristo kupitia sisi kwa kutokua wabinafsi, kuwa na upendo, wenye kujali, kujinyima kwa manufaa ya watu wengine na wawe wana vutwa kwetu kama siku zote wafanyavyo wanapo tutazama sisi kwa makini, kwasababu sisi sote tu wadhambi, wanaweza wasipendezwe na yale yote wanayo yaona kwetu.

 Hivyo ni lazima sikuzote tuwaelekeze kwa Yesu, katika yeye pekee wanaweza wakaweka tumaini lao pekee. Sisi wengine mapema au baadae twaweza kuwakatisha tamaa.
Soma 1 Wakorintho 3:1-9,1 Wakorintho 5:1.Paulo anashughulikia nini katika kanisa hili?Ni aina gani ya ushuhuda ingeonekana hapa kama watu hawa wangekuwa wamewaalika wengine katika kanisa lao na kuona kile ambacho Paulo alikizungumza?
Kwa hakika hatuwezi kuwa wakamilifu, au kuwa na kanisa kamilifu kabla ya kutafuta kuwahudumia wengine. Na wakati huo huo,tunapaswa kutafuta kuwa watu wa aina Fulani ambao ni waaminifu na wengine waweze kujifunza kupitia sisi. Na tutaweza kufanya hivyo tu kwa kuwa waaminifu na wenye kuwajali wengine kama Yesu alivyofanya.Kwa hakika hapana shaka kwamba ugomvi na mapambano ndani ya kanisa yangetokomea kama washiriki wangelenga juu ya kuihudumia jamii na kuufunua kwao upendo wa Kristo.

Kama baadhi ya wageni wangeanza kuhudhuria kanisani kwako kila mara, wangeona nini na ni aina gani ya ushuhuda ungewapatia?

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Sunday, August 28, 2016

Baada ya kuwatakia yaliyo mema, kuwaonesha huruma na kuhudumia mahitaji yao, Yesu “aliishinda Imani yao” Kujiamini (confidence) katika lugha ya kilatini, huundwa na maneno con, maana yake ‘Imani’ Katika Biblia maneno mbalimbali yamejaribu kuelezea maana ya karibu ya neno Imani.

Katika lugha ya Kiebrania mzizi mkuu wa neon Imani ni AMN ambao kwakupitia hilo tunapata neon amina. Wazo la msingi ni kwamba ni la uthabiti na mwendelezo wa kutegemea. Inatupatia wazo la kitu madhubuti, imara ambalo mtu mmoja anaweza kusadiki na kuamini. Mara nyingi hutafsiriwa kama “kuamini” katika muktadha wa Imani ya Mungu yenye kuokoa, na kwa namna nyingine humaanisha “kweli”. Katika muktadha wa mifano ya Kristo katika kushinda Imani za watu, maana yake ilikua kwamba kuamsha aina flani ya Imani ambayo inaonekana kutokua na mashaka yoyote na yenye kujidhatiti, ambayo kwa Yesu ilikua ni kwa kupitia kuchangamana, kuhurumia wenye mahitaji na kuwahudumia watu.
Soma mafungu yafuatayo, ambayo yote yana msingi katika mzizi wa neno AMN (Mwanzo 15:6, Hesabu 14:11, Isaya 7:9, Habakuki 2:4). Imetumikaje katika aya hizi ni kwa jinsi gani linafikisha wazo la kujitumainia na imani?
Katika kiyunani cha agano jipya, mzizi wa neno unaotumika kufikisha kwa kiebrania neno AMN (Imani) ni “pistis” neno hili la kigiriki la Imani humaanisha, Imani,tumaini,uhakika kamili kutumainiwa na neno hili la kigiriki la Imani humaanisha, Imani,tumaini,uhakika kamili kutumainiwa. Katika muktadha wa mifano ya Kristo ya kuzishinda Imani za watu mwonekano waweza kuwa ule wa kuamsha uhakika kamili, Imani , na kuamini katika kukabiliana na kwake na kutokuwa na ubinafsi kwa kujichanganya, na kuhurumia na kuwahudumia.

Ni muhimu kutambua kwamba katika maandiko, popote pale dhana hii ya kujiamini hutokana na binadam, kama katika kujiamini au Imani ya mtu ni mara nyingi huwa na maana mbaya (soma Mika 7:5 na Zaburi 118:9). Huwa na matokeo chanya endapo kujiamini huku kunatokana na Mungu, hili hututahadharisha kama wafuasi waYesu, tumeitwa kuishi kufuatana na mfano wake wa kujichanganya, kuhurumia, na kuwahudumia walio wahitaji. Hata hivyo wakati wale tunao wahudumia wanaonesha kututumainia sisi, nilazima tuwaelekeze kwa Yesu na kile alicho kifanya kwaajili yao.
Kama mtu angejiuliza, “je, Imani ya kweli katika Mungu huonekanaje?” ungejibuje swali hili, na kwanini? Leta jibu lako siku ya sabato

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Saturday, August 27, 2016

 
Sabato Mchana

Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili: Mwa. 15:6, Hes. 14:11, 1 Kor. 3:1–9, Dan. 6:1–3, Neh. 2:1–9, Kum. 4:1–9, Mdo. 2:42–47

Fungu la Kukariri: “‘Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.’” (Luka 5: 15).

Kwa miaka kadhaa, Kanisa la Waadventista Wasabato katika eneo Fulani lilikuwa likitoa kifungua kinywa kwa muda wa siku tano kwa juma katika shule ya awali ya eneo lile.

 Ingawa serikali ya nchi ile haikuwa ya kidini, lakini ilipitisha sheria kutoa pesa kwa kila shule ya serikali ili kuwa na mchungaji, shule pamoja na jamii walilitaka kanisa la Waadventista kutoa mwalimu na Mchungaji mmoja, ni nadra sana kuliomba dhehebu moja tu kufanya hivyo. Jukumu la Mchungaji ni kuwasaidia wanafunzi na jamii nzima ya hapo shuleni, mahitaji ya kimwili, Kihisia, na kiroho. Fursa hii ilikua yakushangaza.

“ Nina furahia uhusiano wa kipekee na maalumu tulionao na kanisa lako,” Mkuu wa shule alimwambia Mchungaji ambaye alikuwa akiitembelea shule, “ Natamani madhehebu mengine, yafanye kama unavyofanya.” Wakati Mchungaji alipokuwa anaondoka katika jamii ile, Afisa Uhusiano wa shule ile alimshukuru kwa kile kanisa lilichokua likifanya na kumuomba kama angeweza kuhudhuria Sabato moja.

Juma hili tutachunguza suala la kuishinda Imani ya watu ambao sisi tunahitaji kuwahudumia na kuwaleta kwa Kristo.
Somo la juma hili limetafsiriwa na Naetwe E.Kimweri pamoja na Agape P. Mrindoko.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA