Baada ya kuwatakia yaliyo mema, kuwaonesha huruma na
kuhudumia mahitaji yao, Yesu “aliishinda Imani yao” Kujiamini
(confidence) katika lugha ya kilatini, huundwa na maneno con, maana yake
‘Imani’ Katika Biblia maneno mbalimbali yamejaribu kuelezea maana ya
karibu ya neno Imani.
Katika lugha ya Kiebrania mzizi mkuu wa neon Imani ni AMN
ambao kwakupitia hilo tunapata neon amina. Wazo la msingi ni kwamba ni
la uthabiti na mwendelezo wa kutegemea. Inatupatia wazo la kitu
madhubuti, imara ambalo mtu mmoja anaweza kusadiki na kuamini. Mara
nyingi hutafsiriwa kama “kuamini” katika muktadha wa Imani ya Mungu
yenye kuokoa, na kwa namna nyingine humaanisha “kweli”. Katika muktadha
wa mifano ya Kristo katika kushinda Imani za watu, maana yake ilikua
kwamba kuamsha aina flani ya Imani ambayo inaonekana kutokua na mashaka
yoyote na yenye kujidhatiti, ambayo kwa Yesu ilikua ni kwa kupitia
kuchangamana, kuhurumia wenye mahitaji na kuwahudumia watu.
Soma mafungu yafuatayo, ambayo yote yana msingi katika
mzizi wa neno AMN (Mwanzo 15:6, Hesabu 14:11, Isaya 7:9, Habakuki 2:4).
Imetumikaje katika aya hizi ni kwa jinsi gani linafikisha wazo la
kujitumainia na imani?
Katika kiyunani cha agano jipya, mzizi wa neno unaotumika
kufikisha kwa kiebrania neno AMN (Imani) ni “pistis” neno hili la
kigiriki la Imani humaanisha, Imani,tumaini,uhakika kamili kutumainiwa
na neno hili la kigiriki la Imani humaanisha, Imani,tumaini,uhakika
kamili kutumainiwa. Katika muktadha wa mifano ya Kristo ya kuzishinda
Imani za watu mwonekano waweza kuwa ule wa kuamsha uhakika kamili, Imani
, na kuamini katika kukabiliana na kwake na kutokuwa na ubinafsi kwa
kujichanganya, na kuhurumia na kuwahudumia.
Ni muhimu kutambua kwamba katika maandiko, popote pale
dhana hii ya kujiamini hutokana na binadam, kama katika kujiamini au
Imani ya mtu ni mara nyingi huwa na maana mbaya (soma Mika 7:5 na Zaburi
118:9). Huwa na matokeo chanya endapo kujiamini huku kunatokana na
Mungu, hili hututahadharisha kama wafuasi waYesu, tumeitwa kuishi
kufuatana na mfano wake wa kujichanganya, kuhurumia, na kuwahudumia
walio wahitaji. Hata hivyo wakati wale tunao wahudumia wanaonesha
kututumainia sisi, nilazima tuwaelekeze kwa Yesu na kile alicho kifanya
kwaajili yao.
Kama mtu angejiuliza, “je, Imani ya kweli katika Mungu
huonekanaje?” ungejibuje swali hili, na kwanini? Leta jibu lako siku ya
sabato****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment