Monday, June 12, 2017
Tuesday, March 28, 2017

Isaya 54:10 "Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali WEMA wangu HAUTAONDOKA kwako, wala AGANO langu la AMANI halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye".
Rafiki; bila kujali hali ya maisha unayoipitia, changamoto zisizoisha, huenda unaomba Maombi na Mungu anaonekana amekaa Kimya - Neno linasema WEMA wa Mungu HAUTAONDOKA KWAKO.  
Kumbuka maisha ya nyuma uliyopitia, ni hakika kuna wakati mgumu ulikuwa mbele yako ukiwa umekosa matumaini, lakini leo hii imebaki kuwa historia. Inua macho yako juu, tazama ahadi za Mungu wako - Naye atalitimiza Neno lake kwa wakati usioudhani. Songa mbele kwa IMANI isiyoyumba, naye ATATENDA.
NAKUTAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE
Na: 
Ev. Eliezer Mwangosi
+255766992265

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Sunday, March 26, 2017****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, March 14, 2017


Friday, March 10, 2017

 VIJANA WENZANGU INATOSHA!
Inatosha Kabisa Sisi Vijana Unafiki Tunaoendekeza Kanisani
>watu Kuunda Tuvikundi Mbalimbali Vya Uimbaj, mara kikundi hiki mara kile Wakat Ndani Yake Wanataka Tu Kuonekana, Na Ndani Yake Yamejaa Mashindano Na Roho Ya Uzinzi, Na Ukifika Wakat Wa Mahubiri Wengi Hutoka Nje Au Kusinzia Tu, Hata Asiposinzia Yeye Ni Kubonya Cmu.INATOSHA Tubadilike
>kumiliki Simu Kubwa, Na Mavaz YaThaman Lakn Unakakosa Biblia,lesson Na Vitabu Vya Nyimbo Kwa Madai Eti Yapo Ndan Ya Cm, Wakat Kanisan Unaishia Kuingia Fb Au Wasap Tu INATOSHA Tubadilike
>wengine Kuwa Nakabiblia Kadogo Nako Kaagano Jipya Tu Na Anakaweka Mfuko Wa Nyuma Na Mpaka Anarud Hakasomi Maana Ni Aibu. Sasa INATOSHA
>Na Wengine Wana Biblia,lesson,nk Lakn Hawasomi Leson Wanachangia Kiuzoefu Unafik Kama Huo INATOSHA!
>Kupenda UimbajNa Mikusanyiko Ya VijanaTu, Wakat Kaz Za Kanisa Hatujitoi Pamoja Nakutotoa Zaka, Lakn Changizo Lakutoa CdYenu Mnatoa HataLak 3 INATOSHA
>japo Sio Wote MUNGUWANGU AMBAYENDIYE MUNGWENU AWABARIKI

Na Esau Msyata

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
 Naomba majina yako kamili:
*Jimson Joseph Mlowe*


Unaimba sauti ya ngap?
*Baritone na backup vocal*

Je ni lini ulianza kuimba sauti hyo?
*Mwaka 2002* *Ila kuanza kuimba ndani Sonda ya Dihlu ni tangu kundi linaanza (I mean ni miongoni mwa founders of the group)*

Katika maisha yako ya kimziki je nini unakipenda kwa kikundi cha Sonda?
*Umoja, uvumilivu na unyenyekevu*

Unapata faida gani kuwepo kati ya waimbaji wa sonda?
*Kukua kiroho na kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii*


Je ukiwa nje ya sonda vitu gan unavimis, nje kwa maana ya safar au sehem nje ya mahali waimbaji wenzako walipo na upo peke yako?
*Combination kwa ujumbe kwa sababu nakuwa najiona siko sawa kwa kiasi flani*
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Thursday, March 09, 2017


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

 Waimbaji wa Ambassadors Of Christ wamefanya kazi kubwa ya injili kwa muda mrefu lakini mwezi wa February wameweza kuzindua DVD yao namba 14 ya HOSIYANA na kwa hakika Bwana ameendelea kuwapigania kwa hili, na katika mtandao wa Facebook wa mmoja wa waimbaji wao KJ Marcello Velosco aliandika maneno haya;-

" DVD MPYA 📀 sasa inapatikana ...Dvd 📀14 ya  jina la HOSIYANA na sasa inapatikana kwenye soko.NI KIPI CHA KIPEKEE KUHUSU DVD HII 📀?Ni kweli kwanza tumefanya mradi wenye nyimbo zikiwa kwenye lugha mbalimbali. Na nyimbo 6 ni za kiswahili, 2 Kinyarwanda nyimbo, 1 Kifaransa wimbo, 1 Lingala wimbo, na 1 Luo wimbo. Sisi kweli khushughulikia mahitaji ya wetu kwani hutofautina , sisi tunajitahidi kuchukua injili kwa watu wote, mataifa na lugha.JINA LA ALBUM NI NINI?Ni jina la HOSIYANA ni tafsiri ya kiswahili na ya Kinyarwanda ni Hoziana. Kwahakika utapenda toleo hili jipya la DVD hii lilivyotengenezwa, na kwa uhakika litabariki mioyo yenu.Unaweza kupata wapi VIDEO?Kwa sasa dvds zinapatikana katika nchi ya Tanzania Daresalaam. kwa wasambazaji waliochuliwa maalum anwani na namba za simu zinapatikana kwenye moja ya miundo ya  picha za makava ya DVD hii. Hivyo, kwa watu wetu wote nchini Tanzania, unaweza kupata nakala. marudio ijayo itakuwa Kigali-Rwanda katika mwezi wa Aprili."
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, March 07, 2017

Tunamengi tungependa kuyajua juu ya waimbaji wa Sonda Ya Dihlu, mara kadhaa tunawaona tu kwenye huduma lakini naamini kuna mambo hatuyajui juu yao hata na huduma kwa ujumla, leo tutasikia haya machache toka kwa muimbaji Elisha Peter na yeye anaimba sauti ya PILI.

 Naitwa Eliya Peter King'wena Ninaimba Sauti ya 2,  Mwaka 2011 Ndo nilianza rasmi kuimba Sonda ya Dihlu katika maisha yangu yamziki ninacho kipenda ndani ya Kundi ni kuimba tu, Faida ninayopata nikuwa karibu na Mungu kumbuka hii ni Ibada hivyo basi unapokuwa ndani lazma tu utakuwa karibu na Mungu. 
                          ----------------------------------------------------------------
 Kiukweli ninacho kimisi kikubwa sana ukiacha kuimba ndani ya Kundi ni  Picnic ukiniuliza huwa tunaenda  kufanya nini, ni Kuogelea kukimbia kidali na kupata marafiki wasio waadventista kwa njia ya kuimba.
 Pia utani Mara kazaa tukienda Elisha na Isaya huwa wao wanapendelea sana kula Ugali kipindi cha chakula wakati huo Mimi Chips mayai, kitu kinaitwa Mishikaki,kachumbali na chumvi kwambali so huwa Nawahesabia matonge ya Ugali kila mtu .
 Pia sauti yangu ninayoimba inatija kwa kikundi, japo ninaimba sauti tatu ukitoa bass, nimekuwa nikihudumu kwa sauti hii tangu kipindi cha rafiki yetu marehem Msafiri ambaye tuliimba wote sauti hiyo, na hata alipotutoka bado ninaimba sauti hii ya pili.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Monday, March 06, 2017

Ni wimbo mwingine mpya kutoka Mabalozi wa Kristo (Ambassadors of Christ).
 Huwa YUWAPI? (Mungu yuko wapi?) Tunapoteseka; wimbo mpya ambayo ni kama swali. Hili ni swali zamani kama historia yenyewe ya binadamu isitoshe watu ikiwa ni pamoja na watu wa Mungu kujikuta wenyewe na swali   katikati ya majanga kuwa wao hawawezi kueleza.
                                            ------------------------------------------
 Wimbo anatumia mazingira ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda kuwasilisha swali, "Mungu yuko wapi?" yaliyotokea kwake kuruhusu mambo kama kutisha kama mauaji ya kimbari kutokea? Ili kujibu swali hili la wimbo unaleta mtu mwingine - "Mungu alikuwa wapi, wakati wake wa mwana pekee mateso kama alipokuwa msalabani"? Jibu ni, Yeye alikuwa pale pale kando ya msalaba, O ndiyo, yeye ni haki badala ya kila kuumiza na mateso mtu. Yeye ni si tofauti, yeye anahisi maumivu yao. wimbo anahitimisha kuwa, Sisi watu wa Rwanda walishiriki kikombe cha mateso wakati wa mauaji hayo, lakini Mungu mara zote amekuwa pale pamoja nasi, wakati wote, na katika wakati muafaka, Yeye alikuja  kwa ajili yetu, kupona na kurejeshwa kwetu, kubadilishwa kwetu kutokana na maumivu na kukata tamaa. Na leo tuna hadithi mpya, hadithi nzuri ya mabadiliko heri ... na O baraka jina lake

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693*******TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Sunday, March 05, 2017


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Haya ni matokeo ya mahubiri ya majuma matatu ya ushindi hatimaye na hawa ni wachungaji waliomkubali Bwana kwa njia ya ubatizo na japo kulikuwa na changamoto kiasi gani. Tazama video hapa chini  wakitoa shuhuda zao. 


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Saturday, March 04, 2017

Na JAMES NGAI, DOHA
 Watu 4 walipata kumpokea Bwana kwa njia ya ubatizo baada ya mahubiri ya kawaida ya kila ibada ya jumamosi na ubatizo huu ulifanywa na Mchungaji Israel Muyiwa toka Nigeria mapema leo

Historia ya kanisa hili kwa ufupi
Ghuba ya Fildi ya kanisa la waadventista wa Sabato ilianzishwa (mahali kanisa lilipo) Mei 20, 2011 kama matokeo ya kuunganisha Ghuba Sehemu ya Afrika (inahusu sehemu za nchi mbili, ambazo ni;-(Falme za Kiarabu na Usultani wa Oman) pamoja na Ghuba Sehemu ya Kaskazini (inayojumuisha Kuwait, Bahrain na Qatar). Eneo hilo lina makanisa 14, na wengi wao wako katika Falme za Kiarabu.****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Friday, March 03, 2017

ITAZAME VIDEO HII HAPA CHINI


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
 Kwenye kila mafanikio changamoto hazikosi, waimbaji wa Sonda ya Dihlu wakati wa kutengeneza album yao ya pili walipata changamoto ya kifedha ambayo iliwapelekea kukosa fursa ya kwenda studio na kuifanya kazi hiyo.
Ilionekana changamoto lakini kwa upande mwingine ilikuwa ni fulsa.
                                                     ------------------------------------
  Bwana ni mwema kwani mmoja wa waimbaji wao ambaye ndiye anasolo nyimbo karibia zote, Mr Isaya alikuwa na studio ndogo ya nyumbani na wala haikuwa na vifaa vya kisasa lakini maajabu ni kwamba kazi ilitoka vizuri nakala nyingi sana zilinunuliwa na Bwana akainuliwa.
 ISIKILIZE AUDIO YA HALELUYA HAPA CHINI
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Kwa mila na desturi zetu tangu kale na kale tumezoea ni ngumu mdada kumwambia kijana anampenda
Njia rahisi hii hapa!
1.jitoe kwa Mungu kwanza,naye atakupatia hekima na maarifa ktk kufanikisha jambo hili,
RUTHU 3:1-3

2.Fanya urafiki naye kwa heshima msalimie kwa adabu wakati fulani anamzigo jaribu kumsaidia.
3.Jitahidi kuonana naye Mara kwa Mara aidha kazini,kanisani,-mtembelee lakini ziwe sehemu za wazi.
4.Jenga urafiki na rafiki yake kipenzi wa yule kijana,ambao utakuwa wenye nidhamu,pia au Dada wa kijana
5.Mtafute mama wa makamo ambaye ni wa heshima ;wanayeheshimiana na yule kijana,kisha jenga urafiki naye-mwisho uwe wazi kwa mama yule.
6.Mpende sana mama wa kijana na baba yake msalimie unapokutana naye,uwe radhi kumsaidia mzigo unapokutana naye.
7.Jiepushe sana kupayukapayuka mipango yako ni siri yako na Mungu ISAYA 41:21.
8.Mtumia kadi za pongezi kama birthday au ushindi wa jambo fulani, mtihani,cheo,kupata kazi,hata kama kazi ni ya Kanisa,ila usiandike neno lolote la mapenzi.
9.Toa zawadi ambazo si za bei kubwa,lakini ambayo ataithamini,kama ni msomi mnunulie Kitabu kizuri chenye ujumbe mzuri lakini isiwe Mara kwa Mara.
10.Tafiti kile anachopendelea,
11.Uwe na bidii. ya kazi.kama ni shamba Lima sana,kama ni ofisini wahi mapema,Acha mzaha kazini onyesha kujali muda wa kazi.
12.Panga kumsaidia kazi au wasaidie wazazi wake,kama unaishi nao karibu
13.Jifunze kupika chakula kizuri kisha siku moja umwalike,aje na rafiki yake,msiwe wawili peke yenu
14.Uwe msafi wakati wote,vaa nguo za heshima, uwe halisia usipende made in China
15.Jiepushe na marafiki walio na tabia mbaya asije akakuweka ktk kundi moja Amosi3:3
16.Jenga imani kwa Mungu,naye hatakuangusha kamwe.
Kwa hayo machache na mengine Mengi, kwa kijana mwenye nia ya kuoa #Atakuja_online_mwenyewe bila wewe kutamka neno ukaonekana mhuni au MTU wa bei rahisi rahis tu.
Barikiwa na Bwana
Na Catheline Masiko
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Mchungaji David Mmbaga ni mmoja ya watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Bugando ambayo ni moja ya Hospitali kubwa hapa Nchini Tanzania, Iliyojengwa mnamo Mwaka 1972. 
February 28, 2017. Kanisa la Mabatini kwa kushirikiana na mchungaji Mbaga walipeleka vitu mbali mbali ikiwemo vifaa tiba katika Wodi ya Watoto na chumba cha Upasuaji katika Hospitali hiyo.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Blogger Widgets

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA