Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

Friday, March 03, 2017

Mchungaji David Mmbaga ni mmoja ya watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Bugando ambayo ni moja ya Hospitali kubwa hapa Nchini Tanzania, Iliyojengwa mnamo Mwaka 1972. 
February 28, 2017. Kanisa la Mabatini kwa kushirikiana na mchungaji Mbaga walipeleka vitu mbali mbali ikiwemo vifaa tiba katika Wodi ya Watoto na chumba cha Upasuaji katika Hospitali hiyo.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, February 28, 2017

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Thursday, February 23, 2017

Na. Dkt. Taphinez Machibya

Je inategemea mtazamo wa mtu/jamii fulani au ni suala la maadili!?
Mwanamke akikataa kutoa mimba licha kushinikizwa na mume wake ataonekana vipi!?
Kumbuka, Mwanamke mwenye hekima huheshimu dhamiri yake.
Takwimu zinatuonesha kwamba Kila mwaka, zaidi ya mimba milioni 50 hutolewa, na matokeo ni kwamba idadi ya watoto wanaouawa ni kubwa kuliko idadi ya watu katika nchi nyingi.
 
WATU HUSEMA NINI?
Kuna sababu kadhaa zinazofanya baadhi ya wanawake watoe mimba. Sababu hizo zinahusisha:
* Aibu au mtazamo hasi kwa jamii
*Hali mbaya ya kifedha,
*Matatizo katika mahusiano,
*Tamaa ya kuwa huru kuendelea na masomo au kazi, na
*Kutotaka kulea mtoto bila mume.

Hata hivyo, wengine huona kutoa mimba kuwa kosa la kimaadili, yaani, kutotimiza jukumu ambalo mwanamke mjamzito amekabidhiwa.

BIBLIA INASEMA NINI?
Machoni pa Mungu, uhai, hasa uhai wa mwanadamu, ni mtakatifu. (Mwanzo 9:6; Zaburi 36:9) Kanuni hii inatumika hata kwa kiumbe aliye bado tumboni, mahali salama pa ukuaji wa mtoto palipoandaliwa na Mungu.
Mwandishi mmoja wa Biblia alisema hivi: “Uliniweka nikiwa nimekingwa katika tumbo la mama yangu.” Akaongeza hivi: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa, kuhusiana na siku ambazo zilifanyizwa.”—Zaburi 139:13, 16.

Maoni ya Mungu kuhusu uhai yanaonekana pia kwenye Sheria yake kwa taifa la Israeli na kupitia dhamiri aliyotupatia. Sheria ya Mungu ilisema kwamba ikiwa mtu angemshambulia mwanamke mwenye mimba na kusababisha kifo cha mtoto aliye tumboni, angehukumiwa kifo na kuuawa ili kulipia uhai wa yule mtoto. (Kutoka 21:22, 23) Bila shaka, waamuzi wangechunguza nia na mazingira ya tukio kabla ya kutoa hukumu.—Hesabu 35:22-24, 31.
Pia, Mungu amewapatia wanadamu zawadi ya dhamiri, ile sauti ya ndani. Mwanamke atakuwa na dhamiri safi ikiwa ataisikiliza na hivyo kuheshimu uhai wa mtoto ambaye hajazaliwa. Akipuuza dhamiri yake, itamsumbua au hata kumshtaki. (Waroma 2:14, 15).
Utafiti unaonyesha kwamba wanawake waliotoa mimba wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kuwa na wasiwasi kupita kiasi, na kushuka moyo.

Hata hivyo, vipi ikiwa jukumu la kulea mtoto linaonekana kuwa kubwa sana hasa katika hali ya kisa cha mimba zisizotarajiwa? Ona jinsi ambavyo Mungu anawahakikishia wale wanaoshikamana na viwango vyake: “Kwa mtu mshikamanifu utatenda kwa ushikamanifu; kwa mwanamume [au mwanamke] asiye na kosa, wewe utatenda kwa njia isiyo na kosa.” (Zaburi 18:25) Biblia pia inasema: “Yehova ni mpenda-haki, naye hatawaacha waaminifu wake.”—Zaburi 37:28.
“Dhamiri yao [inawatolea] ushahidi na, katikati ya fikira zao wenyewe, wanashtakiwa au hata kutetewa.”—Waroma 2:15.
Namna gani ikiwa uliwahi kutoa mimba?

WATU HUSEMA NINI?
Mama mmoja asiye na mume, alipohojiwa kwa nini alitoa mimba alisema hivi: “Tayari nilikuwa na watoto wadogo watatu, hivyo, nikahisi kwamba nisingeweza kutunza mtoto wa nne. Hata hivyo, baada ya kutoa mimba, nilihisi kwamba nimefanya kosa kubwa sana.”
Je, unadhani huyu mama alikuwa amefanya kosa lisilosameheka machoni pa Mungu?

BIBLIA INASEMA NINI?
Yesu Kristo alionyesha maoni ya Mungu kuhusu suala hilo aliposema hivi: “Nimekuja kuwaita, si watu waadilifu, bali watenda-dhambi ili watubu.” (Luka 5:32) Naam, iwapo tunajuta kikweli kutokana na kosa tulilofanya, tukitubu na kumwomba Mungu msamaha, yeye atatusamehe kwa hiari hata ikiwa tulifanya dhambi nzito. (Isaya 1:18) Andiko la Zaburi 51:17 linasema: “Moyo uliovunjika na kupondwa, Ee Mungu, hutaudharau.”

Pamoja na kuwa na dhamiri safi, Mungu anampatia mtu aliyetubu amani ya akili atakapomwomba kwa unyenyekevu kupitia sala. Andiko la Wafilipi 4:6, 7 linasema hivi: “Kwa sala na dua pamoja na kutoa shukrani maombi yenu na yajulikane na Mungu; na amani ya Mungu yenye ubora unaozidi fikira zote itailinda mioyo yenu na nguvu zenu za akili.”
Baada ya kujifunza Biblia na kumimina moyo wake kwa Mungu, mama huyu alipata amani ya akili. Alijifunza kwamba kwa Mungu “kuna msamaha wa kweli.”—Zaburi 130:4.

SAYANSI INASEMA NINI!?
"Nyakati nyingine afya ya mama na au mtoto inaweza kuwa hatarini. Lakini hiyo haipaswi kuwa sababu ya kutoa mimba. Uahi ni swala nyeti sana jamani. Ikitokea kwamba wakati wa mimba au kujifungua hali inalazimu mmoja kati ya mama au mtoto apoteze uhai, hilo ni jukumu la wenzi wa ndoa na wataalamu wa afya kuamua. Lakini tunamshukuru Mungu kwamba maendeleo ya tiba hasa katika tasnia ya afya yamefanya visa vya aina hii kupungua sana. Ikitokea na ikalazimu hebu hekima ya Mungu na itutangulie katika swala hili la Kufa na kupona.

“[Mungu] hakututendea kulingana na dhambi zetu; wala kuleta juu yetu kile tunachostahili kulingana na makosa yetu.”—Zaburi 103:10.
Hiyo ndiyo maana ya neema.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Wednesday, February 15, 2017

"KUTOA MIMBA."
Je inategemea mtazamo wa mtu/jamii fulani au ni suala la maadili!?
Mwanamke akikataa kutoa mimba licha kushinikizwa na mume wake ataonekana vipi!?
Kumbuka, Mwanamke mwenye hekima huheshimu dhamiri yake.
Takwimu zinatuonesha kwamba Kila mwaka, zaidi ya mimba milioni 50 hutolewa, na matokeo ni kwamba idadi ya watoto wanaouawa ni kubwa kuliko idadi ya watu katika nchi nyingi.
WATU HUSEMA NINI?
Kuna sababu kadhaa zinazofanya baadhi ya wanawake watoe mimba. Sababu hizo zinahusisha:
* Aibu au mtazamo hasi kwa jamii
*Hali mbaya ya kifedha,
*Matatizo katika mahusiano,
*Tamaa ya kuwa huru kuendelea na masomo au kazi, na
*Kutotaka kulea mtoto bila mume.

Hata hivyo, wengine huona kutoa mimba kuwa kosa la kimaadili, yaani, kutotimiza jukumu ambalo mwanamke mjamzito amekabidhiwa.
BIBLIA INASEMA NINI?
Machoni pa Mungu, uhai, hasa uhai wa mwanadamu, ni mtakatifu. (Mwanzo 9:6; Zaburi 36:9) Kanuni hii inatumika hata kwa kiumbe aliye bado tumboni, mahali salama pa ukuaji wa mtoto palipoandaliwa na Mungu.
Mwandishi mmoja wa Biblia alisema hivi: “Uliniweka nikiwa nimekingwa katika tumbo la mama yangu.” Akaongeza hivi: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa, kuhusiana na siku ambazo zilifanyizwa.”—Zaburi 139:13, 16.

Maoni ya Mungu kuhusu uhai yanaonekana pia kwenye Sheria yake kwa taifa la Israeli na kupitia dhamiri aliyotupatia. Sheria ya Mungu ilisema kwamba ikiwa mtu angemshambulia mwanamke mwenye mimba na kusababisha kifo cha mtoto aliye tumboni, angehukumiwa kifo na kuuawa ili kulipia uhai wa yule mtoto. (Kutoka 21:22, 23) Bila shaka, waamuzi wangechunguza nia na mazingira ya tukio kabla ya kutoa hukumu.—Hesabu 35:22-24, 31.
Pia, Mungu amewapatia wanadamu zawadi ya dhamiri, ile sauti ya ndani. Mwanamke atakuwa na dhamiri safi ikiwa ataisikiliza na hivyo kuheshimu uhai wa mtoto ambaye hajazaliwa. Akipuuza dhamiri yake, itamsumbua au hata kumshtaki. (Waroma 2:14, 15).
Utafiti unaonyesha kwamba wanawake waliotoa mimba wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kuwa na wasiwasi kupita kiasi, na kushuka moyo.

Hata hivyo, vipi ikiwa jukumu la kulea mtoto linaonekana kuwa kubwa sana hasa katika hali ya kisa cha mimba zisizotarajiwa? Ona jinsi ambavyo Mungu anawahakikishia wale wanaoshikamana na viwango vyake: “Kwa mtu mshikamanifu utatenda kwa ushikamanifu; kwa mwanamume [au mwanamke] asiye na kosa, wewe utatenda kwa njia isiyo na kosa.” (Zaburi 18:25) Biblia pia inasema: “Yehova ni mpenda-haki, naye hatawaacha waaminifu wake.”—Zaburi 37:28.
“Dhamiri yao [inawatolea] ushahidi na, katikati ya fikira zao wenyewe, wanashtakiwa au hata kutetewa.”—Waroma 2:15.
Namna gani ikiwa uliwahi kutoa mimba?
WATU HUSEMA NINI?
Mama mmoja asiye na mume, alipohojiwa kwa nini alitoa mimba alisema hivi: “Tayari nilikuwa na watoto wadogo watatu, hivyo, nikahisi kwamba nisingeweza kutunza mtoto wa nne. Hata hivyo, baada ya kutoa mimba, nilihisi kwamba nimefanya kosa kubwa sana.”
Je, unadhani huyu mama alikuwa amefanya kosa lisilosameheka machoni pa Mungu?

BIBLIA INASEMA NINI?
Yesu Kristo alionyesha maoni ya Mungu kuhusu suala hilo aliposema hivi: “Nimekuja kuwaita, si watu waadilifu, bali watenda-dhambi ili watubu.” (Luka 5:32) Naam, iwapo tunajuta kikweli kutokana na kosa tulilofanya, tukitubu na kumwomba Mungu msamaha, yeye atatusamehe kwa hiari hata ikiwa tulifanya dhambi nzito. (Isaya 1:18) Andiko la Zaburi 51:17 linasema: “Moyo uliovunjika na kupondwa, Ee Mungu, hutaudharau.”

Pamoja na kuwa na dhamiri safi, Mungu anampatia mtu aliyetubu amani ya akili atakapomwomba kwa unyenyekevu kupitia sala. Andiko la Wafilipi 4:6, 7 linasema hivi: “Kwa sala na dua pamoja na kutoa shukrani maombi yenu na yajulikane na Mungu; na amani ya Mungu yenye ubora unaozidi fikira zote itailinda mioyo yenu na nguvu zenu za akili.”
Baada ya kujifunza Biblia na kumimina moyo wake kwa Mungu, mama huyu alipata amani ya akili. Alijifunza kwamba kwa Mungu “kuna msamaha wa kweli.”—Zaburi 130:4.

SAYANSI INASEMA NINI!?
"Nyakati nyingine afya ya mama na au mtoto inaweza kuwa hatarini. Lakini hiyo haipaswi kuwa sababu ya kutoa mimba. Uhai ni swala nyeti sana jamani. Ikitokea kwamba wakati wa mimba au kujifungua hali inalazimu mmoja kati ya mama au mtoto apoteze uhai, hilo ni jukumu la wenzi wa ndoa na wataalamu wa afya kuamua. Lakini tunamshukuru Mungu kwamba maendeleo ya tiba hasa katika tasnia ya afya yamefanya visa vya aina hii kupungua sana. Ikitokea na ikalazimu hebu hekima ya Mungu na itutangulie katika swala hili la Kufa na kupona.

“[Mungu] hakututendea kulingana na dhambi zetu; wala kuleta juu yetu kile tunachostahili kulingana na makosa yetu.”—Zaburi 103:10.
Hiyo ndiyo maana ya neema.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Tuesday, January 03, 2017

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Wednesday, November 16, 2016

Na Conges Mramba,Mwanza

Hospitali ya Wasabato Pasiansi mbioni kukamilika HOSPITALI ya wa-Adventista wa Sabato, iitwayo Mwanza Adventist Medical Centre(MAMC) ikikamilika kujengwa itakuwa imegharimu takriban shilingi bilioni tatu.
Mkurugenzi wa Afya na Kiasi wa Jimbo la Nyanza Kusini(SNC)Dk.Baraka Musa Maginga, alisema siku zilizopita kwamba kama washiriki wangetoa michango na sadaka zao kwa uaminifu, Hospitali hiyo iliyoko Pasiansi jijini Mwanza, ingeanza huduma katikati ya Julai mwaka huu 2016,kwa kuwa tayari vifaa vingi vipo.
Akizungumza nami katika Kanisa la Kirumba,jijini Mwanza,Dk. Maginga aliyekuwa akihimiza washiriki kutoa sadaka ya ujenzi wa Hospitali hiyo amesema MAMC itaanza kuhudumia wagonjwa kwa kutumia eneo la chini(Ground Floor) la jengo hilo na gorofa ya kwanza.
Amesema, hadi sasa kazi inayoendelea kufanywa ni pamoja na uwekaji wa madirisha,kupanga rangi na kuweka kingo za nje.
Aidha,Daktari huyo amesema serikali ilikuwa imewaruhusu Hospitali hiyo kuanza katika vyumba vya chini vya jingo hilo jipya,kwa kuwa hata sasa kuna huduma zinazoendelea kufanywa na kituo cha Afya.
Akizungumzia vifaa tiba, matabibu na madaktari,amesema vifaa vipo tayari na madaktari wapo wa kutosha kuanza kutoa huduma ifikapo Julai mwaka huu ambako amesema vyumba vitakavyokuwa tayari katika jengo hilo jipya vitaweza kuwekwa vifaa tiba kama mashine ya mionzi(X-ray),chumba cha upasuaji na Ultra Sound.
Hadi sasa Hospitali hii ya MAMC imetumia shilingi bilioni 1.9 ambazo ni michango na sadaka za wauamini; na itakapokamilika baadaye inatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu.
Hospitali hii itaanza na jumla ya vitanda 100 vya kulaza wagonjwa hususan akina mama wajawazito watakaofika hospitalini hapo kujifungua.
Dk.Maginga amesema hospitali hiyo itafunguliwa baadaye mwaka huu na baadaye itakuwa na vyuo vya tiba,maabara na wafamasia.
Baadaye,MAMC inatazamiwa kuwa na jumla ya vitanda 450 vya kilaza wagonjwa,wakati zaidi ya wagonjwa 200 wa Nje(OPD) wakitibiwa kila siku na kuondoka.
Hadi sasa jiji la Mwanza lina Hospitali tatu za rufaa, hivyo MAMC itakapoanza rasmi kufanya kazi itakuwa inapunguza mrundikano wa wagonjwa katika Hospitali ya Bugando ambayo ina jumla ya vitanda 950 vya kulaza wagonjwa.
Hospitali nyingine zilizoko Mwanza ni Sekou Toure,Mwananchi na Nyamagana iliyoko Butimba wilayani Nyamagana.
Hospitali ya Bugando inayomilikiwa na Kanisa Katoliki ilianza mwaka 1972, na ni miongoni mwa Hospitali nne tu za Rufaa katika eneo la Magharibi mwa Tanzania na ukanda wa Ziwa Victoria ambako kuna takriban wakazi milioni 16 kati ya Watanzania milioni 45.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Friday, October 07, 2016

Na Dr. Taphinez  Machibya

 .

Kila jambo lina utaratibu na kanuni zake ili liweze kuwa na matokeo chanya maishani. Vivyo hivyo hata mwili wa binadamu una kanuni zake na hivyo ili tuweze kupata manufaa ya chakula hasa baada ya mlo, yatupasa kuzingatia yafuatayo;

1.       USILE MATUNDA MARA TU BAADA YA KULA: Hii husababisha tumbo kujaa gesi /hewa ambayo huingilia mmeng’enyo wa chakula. Kula matunda saa 1-2 kabla au baada ya kula.

2.       USINYWE CHAI: Kemikali ya Asidi iliyomo katika chai husababisha chakula kugandamana na kushindwa kusharabiwa vema katika kuta za utumbo

3.       USILEGEZE MKANDA( WA NGUO): Hii inaweza kusababisha utumbo kusokotana , kupandana na  kuzibwa kwa njia ya chakula.

4.       USIOGE : Hii itapelekea damu kwenda sehemu za mbali za mwili ili kusawazisha joto vema kama vile mikononi,miguuni,na sehemu zingine za mwili hivyo kudhoofisha umeng’enyaji na wa chakula na uchukuliwaji wa virutubisho vya chakula katika utumbo.

5.       USITEMBEE UMBALI MREFU/KUFANYA KAZI NZITO /MAZOEZI : Hii husababisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kushindwa kufyonza virutubisho toka tumboni kwa sababu ya mvurugano wa shughuli zinazofanywa  na mhusika.

6.       USIVUTE SIGARA: Kwa sababu mwili unafyonza chakula wakati huu,utafiti unaonyesha kwamba kuvuta sigara moja (1) baada ya kula ni sawa na mtu aliyevuta sigara 10,hivyo kuongeza uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kansa haraka zaidi.

7.       USILALE MAPEMA: Kulala mara tu baada ya kula hubana misuli ya tumbo na kuzuia chakula kisitembee sawia tumboni,hii hupelekea maambukizi na magonjwa ya tumbo na utumbo kwa sababu chakula huishia kuozea tumboni na kuruhusu wadudu wa magonjwa mbalimbali kustawi vema.

Hivyo ili tuweze kula kwa faida na chakula kiwe cha manufaa mwilini baada ya kuliwa ni vema tukiyazingatia hayo!

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Friday, September 30, 2016

Na Dr. Taphinez Machibya

.
MAANA.
       Kuhara maana yake ni kuharisha au kupitisha kinyesi chenye damu.
       Hutokea hasa wa watoto chini ya miaka mitanoi
       Kinyesi chaweza uwa na damu nyingi au kidogo au nyingi au kuwa na vitu kama kamasi kamasi hivi.
TAKWIMU:
       Magonjwa ya kuhara ni ya pili katika uuaji wa watoto duniani kote.
       Shirika la afya duniani WHO, linaonesha kila mwaka zaidi ya watoto 700,000 wenye umri chini ya miaka 5 hufa kwa magonjwa ya kuhara.
       Magonjwa haya yanazuilika kwa njia mbalimbali.
SABABU ZA KUHARA
       Maambukizi ya vimelea kama bacteria (e.coli, shigella, etc), virusi (rotavirus)na protozoa(entamoeba histolytica, Giardiasis, B. coli).
       Magonjwa kama ukimwi
       Utapiamlo
       Magonjwa ya UTI,
       Baadhi ya madawa
UENEAJI NA MAAMBUKIZI.
       Magonjwa ya kuhara yako ya aina nyingi, mengine siyo ambukizi lakini mengine ni ya kuambukiza .
       Mfano ni homa ya Matumbo(Typhoid fever), kipindupindu (Cholera), kuhara damu (dysentery) ,minyoo aina mbalimbali n.k
       Magonjwa haya husambaa kwa ulaji wa kinyesi kwa njia tofauti,kama vile:
Ø  Kula chakula bila kuosha mikono
Ø  Kunywa maji yasiyo salama (chemshwa)
Ø  Nzi,mende na wadudu wengine kutua kwenye kinyesi kisha kutembelea chakula
Ø  Kunyonya vidole visivyo safi n.k
Ø  Chupa za kunyonyeshea  zisizo fanyiwa  usafi au matiti ya mama yasiyo safi.
TABIA ZA WADUDU WA MAGONJWA YA KUHARA.
       Kufahamu tabia za wadudu wa kuhara husaidia kuelewa jinsi ya kujikinga na kukinga watoto dhidi ya magonjwa.
       Wadudu wengi wa magonjwa ya kuhara huwa na tabia zifuatazo;
ü  Hawaonekani kwa macho
ü  Huweza kukaa kwenye chakula na mabaki ya chakula bila kufa zaidi ya siku 4, hukaa kwenye maji zaidi ya siku 11, na kwenye kinyesi ama nguo au nepi zenye kinyesi kwa zaidi wiki 7.
ü  Hubebwa na kusambazwa kirahisi na nzi,mende n.k
ü  Huzaliana kwa haraka sana (ndani ya masaa machache wadudu huweza kuwa mamilioni)
ü  Hufa kwa joto la juu kuanzia 60 C , ama kwa madini ya Chlorine.
JINSI YA KUWALINDA WATOTO NA WANAFAMILIA.
       Matumizi sahihi ya vyoo. Kinyesi cha wanafamilia rika zote hata watoto kitupwe kwa usahihi chooni.
       Vyoo vifanyiwe usafi na kupigwa dawa (fumigation) kuondoa nzi, mende, na wadudu watambaao na kuruka wanaoweza kusambaza magonjwa.
       Kila mwanafamilia kuosha mikono kila baada ya kutumia choo, na kabla ya kuandaa chakula ama  baada ya kula.
       Kuhifadhi chakula sehemu salama na safi
       Kupasha chakula vizuri kabla ya kutumia
       Kutumia maji safi na salama kwa kunywa, kutengenezea juisi, kusafishia ,matunda na mboga zinazoliwa zikiwa mbichi, kuosha chupa  za  chakula cha mtoto.
       Maji safi hufanywa kuwa salama kwa kuchemshwa hadi kutokota ama kuweka madini ya chlorine.
       Kunyonyesha bila kuchanganya na chakula kwa miezi 6 ya kwanza ya mtoto,Maziwa ya mama yana kinga dhidi ya baadhi ya magonjwa, Maziwa haya kwa miezi 6 ya kwanza ni lishe kamili na toshelezi kwa mtoto.
       Kuwapatia watoto lishe ama mlo kamili wenye Protini, wanga , vitamini ,mafuta, madini na nyuzinyuzi. Lishe bora huongeza kinga ya mtoto kwa magonjwa ambukizi.
       Kuhudhuria kliniki na kuhakikisha mtoto anapata chanjo zote stahiki kadri  ya umri wa miaka 5.
NINI KIFANYIKE MTOTO ANAPOHARISHA?
       Tafuta kumwona daktari mapema iwezekanavyo , mtoto akihara zaidi ya mara 3 kwa siku 1,ama ukiona damu ama makamasi kwenye kinyesi.
       Mtoto anayehara na kutapika aharakishwe zaidi hospitali.
       Wakati ukitafuta msaada wa daktari hakikisha mtoto hapungukiwi maji mwilini kwa kumpatia ORS na chakula kama kawaida.
       Usimpatie mtoto dawa yoyote bila ushauri wa daktari.
       Msafishe mtoto vizuri kwa maji safi na sabuni kila anapohara na kutupa kinyesi chake vizuri chooni ,nepi zenye kinyesi zinaweza kulowekwa na jiki na kusafishwa kwa sabuni.
 
UNAPOFIKA KWA DAKTARI:
       Uwe na taarifa sahihi juu ya ;
Ø  Lini ama saa ngapi mtoto alianza kuhara.
Ø  Kama anahara na kutapika
Ø  Amehara na kutapika mara ngapi
Ø  Kinyesi chake kinafananaje
Ø  Amepatiwa huduma gani ya kwanza
Ø  Kama yuko kwenye dawa yoyote
Ø  Kama ametoka kupokea chanjo yoyote siku za  karibu.

HITIMISHO:
Kuwalinda watoto wetu na familia zetu dhidi ya magonjwa ambukizi ya KUHARA ni jukumu letu sote. Tutimize wajibu wetu wa kupigana na magonjwa haya,ushindi ni hakika tukifuata taratibu bora za afya!

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA