Na Dr. Taphinez Machibya |
.
Kila jambo
lina utaratibu na kanuni zake ili liweze kuwa na matokeo chanya maishani. Vivyo
hivyo hata mwili wa binadamu una kanuni zake na hivyo ili tuweze kupata manufaa
ya chakula hasa baada ya mlo, yatupasa kuzingatia yafuatayo;
1. USILE MATUNDA MARA TU BAADA YA KULA: Hii husababisha tumbo kujaa gesi /hewa ambayo huingilia mmeng’enyo
wa chakula. Kula matunda saa 1-2 kabla au baada ya kula.
2. USINYWE CHAI: Kemikali ya Asidi
iliyomo katika chai husababisha chakula kugandamana na kushindwa kusharabiwa
vema katika kuta za utumbo
3. USILEGEZE
MKANDA( WA NGUO): Hii inaweza kusababisha utumbo kusokotana , kupandana na kuzibwa kwa njia ya chakula.
4. USIOGE
: Hii itapelekea damu kwenda sehemu za mbali za mwili ili kusawazisha joto vema
kama vile mikononi,miguuni,na sehemu zingine za mwili hivyo kudhoofisha
umeng’enyaji na wa chakula na uchukuliwaji wa virutubisho vya chakula katika
utumbo.
5. USITEMBEE
UMBALI MREFU/KUFANYA KAZI NZITO /MAZOEZI : Hii husababisha mfumo wa mmeng’enyo
wa chakula kushindwa kufyonza virutubisho toka tumboni kwa sababu ya mvurugano
wa shughuli zinazofanywa na mhusika.
6. USIVUTE
SIGARA: Kwa sababu mwili unafyonza chakula wakati huu,utafiti unaonyesha kwamba
kuvuta sigara moja (1) baada ya kula ni sawa na mtu aliyevuta sigara 10,hivyo
kuongeza uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kansa haraka zaidi.
7. USILALE
MAPEMA: Kulala mara tu baada ya kula hubana misuli ya tumbo na kuzuia chakula
kisitembee sawia tumboni,hii hupelekea maambukizi na magonjwa ya tumbo na
utumbo kwa sababu chakula huishia kuozea tumboni na kuruhusu wadudu wa magonjwa
mbalimbali kustawi vema.
Hivyo ili tuweze kula kwa faida na
chakula kiwe cha manufaa mwilini baada ya kuliwa ni vema tukiyazingatia hayo!
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment