Wednesday, February 15, 2017


"KUTOA MIMBA."
Je inategemea mtazamo wa mtu/jamii fulani au ni suala la maadili!?
Mwanamke akikataa kutoa mimba licha kushinikizwa na mume wake ataonekana vipi!?
Kumbuka, Mwanamke mwenye hekima huheshimu dhamiri yake.
Takwimu zinatuonesha kwamba Kila mwaka, zaidi ya mimba milioni 50 hutolewa, na matokeo ni kwamba idadi ya watoto wanaouawa ni kubwa kuliko idadi ya watu katika nchi nyingi.
WATU HUSEMA NINI?
Kuna sababu kadhaa zinazofanya baadhi ya wanawake watoe mimba. Sababu hizo zinahusisha:
* Aibu au mtazamo hasi kwa jamii
*Hali mbaya ya kifedha,
*Matatizo katika mahusiano,
*Tamaa ya kuwa huru kuendelea na masomo au kazi, na
*Kutotaka kulea mtoto bila mume.

Hata hivyo, wengine huona kutoa mimba kuwa kosa la kimaadili, yaani, kutotimiza jukumu ambalo mwanamke mjamzito amekabidhiwa.
BIBLIA INASEMA NINI?
Machoni pa Mungu, uhai, hasa uhai wa mwanadamu, ni mtakatifu. (Mwanzo 9:6; Zaburi 36:9) Kanuni hii inatumika hata kwa kiumbe aliye bado tumboni, mahali salama pa ukuaji wa mtoto palipoandaliwa na Mungu.
Mwandishi mmoja wa Biblia alisema hivi: “Uliniweka nikiwa nimekingwa katika tumbo la mama yangu.” Akaongeza hivi: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa, kuhusiana na siku ambazo zilifanyizwa.”—Zaburi 139:13, 16.

Maoni ya Mungu kuhusu uhai yanaonekana pia kwenye Sheria yake kwa taifa la Israeli na kupitia dhamiri aliyotupatia. Sheria ya Mungu ilisema kwamba ikiwa mtu angemshambulia mwanamke mwenye mimba na kusababisha kifo cha mtoto aliye tumboni, angehukumiwa kifo na kuuawa ili kulipia uhai wa yule mtoto. (Kutoka 21:22, 23) Bila shaka, waamuzi wangechunguza nia na mazingira ya tukio kabla ya kutoa hukumu.—Hesabu 35:22-24, 31.
Pia, Mungu amewapatia wanadamu zawadi ya dhamiri, ile sauti ya ndani. Mwanamke atakuwa na dhamiri safi ikiwa ataisikiliza na hivyo kuheshimu uhai wa mtoto ambaye hajazaliwa. Akipuuza dhamiri yake, itamsumbua au hata kumshtaki. (Waroma 2:14, 15).
Utafiti unaonyesha kwamba wanawake waliotoa mimba wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kuwa na wasiwasi kupita kiasi, na kushuka moyo.

Hata hivyo, vipi ikiwa jukumu la kulea mtoto linaonekana kuwa kubwa sana hasa katika hali ya kisa cha mimba zisizotarajiwa? Ona jinsi ambavyo Mungu anawahakikishia wale wanaoshikamana na viwango vyake: “Kwa mtu mshikamanifu utatenda kwa ushikamanifu; kwa mwanamume [au mwanamke] asiye na kosa, wewe utatenda kwa njia isiyo na kosa.” (Zaburi 18:25) Biblia pia inasema: “Yehova ni mpenda-haki, naye hatawaacha waaminifu wake.”—Zaburi 37:28.
“Dhamiri yao [inawatolea] ushahidi na, katikati ya fikira zao wenyewe, wanashtakiwa au hata kutetewa.”—Waroma 2:15.
Namna gani ikiwa uliwahi kutoa mimba?
WATU HUSEMA NINI?
Mama mmoja asiye na mume, alipohojiwa kwa nini alitoa mimba alisema hivi: “Tayari nilikuwa na watoto wadogo watatu, hivyo, nikahisi kwamba nisingeweza kutunza mtoto wa nne. Hata hivyo, baada ya kutoa mimba, nilihisi kwamba nimefanya kosa kubwa sana.”
Je, unadhani huyu mama alikuwa amefanya kosa lisilosameheka machoni pa Mungu?

BIBLIA INASEMA NINI?
Yesu Kristo alionyesha maoni ya Mungu kuhusu suala hilo aliposema hivi: “Nimekuja kuwaita, si watu waadilifu, bali watenda-dhambi ili watubu.” (Luka 5:32) Naam, iwapo tunajuta kikweli kutokana na kosa tulilofanya, tukitubu na kumwomba Mungu msamaha, yeye atatusamehe kwa hiari hata ikiwa tulifanya dhambi nzito. (Isaya 1:18) Andiko la Zaburi 51:17 linasema: “Moyo uliovunjika na kupondwa, Ee Mungu, hutaudharau.”

Pamoja na kuwa na dhamiri safi, Mungu anampatia mtu aliyetubu amani ya akili atakapomwomba kwa unyenyekevu kupitia sala. Andiko la Wafilipi 4:6, 7 linasema hivi: “Kwa sala na dua pamoja na kutoa shukrani maombi yenu na yajulikane na Mungu; na amani ya Mungu yenye ubora unaozidi fikira zote itailinda mioyo yenu na nguvu zenu za akili.”
Baada ya kujifunza Biblia na kumimina moyo wake kwa Mungu, mama huyu alipata amani ya akili. Alijifunza kwamba kwa Mungu “kuna msamaha wa kweli.”—Zaburi 130:4.

SAYANSI INASEMA NINI!?
"Nyakati nyingine afya ya mama na au mtoto inaweza kuwa hatarini. Lakini hiyo haipaswi kuwa sababu ya kutoa mimba. Uhai ni swala nyeti sana jamani. Ikitokea kwamba wakati wa mimba au kujifungua hali inalazimu mmoja kati ya mama au mtoto apoteze uhai, hilo ni jukumu la wenzi wa ndoa na wataalamu wa afya kuamua. Lakini tunamshukuru Mungu kwamba maendeleo ya tiba hasa katika tasnia ya afya yamefanya visa vya aina hii kupungua sana. Ikitokea na ikalazimu hebu hekima ya Mungu na itutangulie katika swala hili la Kufa na kupona.

“[Mungu] hakututendea kulingana na dhambi zetu; wala kuleta juu yetu kile tunachostahili kulingana na makosa yetu.”—Zaburi 103:10.
Hiyo ndiyo maana ya neema.


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA