Tuesday, March 28, 2017

Isaya 54:10 "Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali WEMA wangu HAUTAONDOKA kwako, wala AGANO langu la AMANI halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye".
Rafiki; bila kujali hali ya maisha unayoipitia, changamoto zisizoisha, huenda unaomba Maombi na Mungu anaonekana amekaa Kimya - Neno linasema WEMA wa Mungu HAUTAONDOKA KWAKO.  
Kumbuka maisha ya nyuma uliyopitia, ni hakika kuna wakati mgumu ulikuwa mbele yako ukiwa umekosa matumaini, lakini leo hii imebaki kuwa historia. Inua macho yako juu, tazama ahadi za Mungu wako - Naye atalitimiza Neno lake kwa wakati usioudhani. Songa mbele kwa IMANI isiyoyumba, naye ATATENDA.
NAKUTAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE
Na: 
Ev. Eliezer Mwangosi
+255766992265

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA