Sunday, June 19, 2022

 Soma Mwanzo 46. Kuondoka kwa Yakobo Kanaani kuna umuhimu gani?

 

Yakobo anapoondoka kwake Kanaani, amejawa tumaini. Uhakikisho kwamba hataona njaa tena, na habari njema kwamba Yusufu yu hai, ni lazima vilimpa msukumo kwamba anapaswa kondoka katika Nchi ya Ahadi.

Kuondoka kwa Yakobo kunatoa mwangwi wa uzoefu wa Ibrahimu, ingawa kwa habari ya Ibrahimu alikuwa anaelekea katika Nchi ya Ahadi. Yakobo anasikia ahadi ile ile ya Ibrahimu ambayo Ibrahimu aliisikia toka kwa Mungu, yaani kwamba atamfanya kuwa “taifa kubwa” (Mwa. 46:3; linganisha na Mwa. 12:2). Wito wa Mungu hapa pia ni ukumbusho wa agano la Mungu na Ibrahimu; katika matukio yote Mungu anatumia neno lile lile linalotoa uthibitisho tena “ ‘usiogope’ ” (Mwa. 46:3; linganisha na Mwa. 15:1), linalobeba ahadi ya maisha yajayo yenye utukufu.

Kuorodheshwa kwa upana kwa majina ya watoto wa Israeli walioenda Misri, pamoja na binti zake (Mwa. 46:7), kunakumbusha ahadi ya Mungu ya uzao mwingi kwa Ibrahimu hata wakati akiwa bado hana mtoto. Namba “sabini” (pamoja na Yakobo, Yusufu, na wanawe wawili) inaelezea wazo la utimilifu/ukamilifu. Ni “Israeli yote” inayokwenda Misri. Ni muhimu pia kwamba namba 70 inafanana na namba ya mataifa (Mwanzo 10), kuashiria kwamba hatima ya mataifa yote ina hatarishwa katika safari ya Yakobo.

Ukweli huu utakuwa dhahiri zaidi tu miaka mingi baadaye, baada ya msalaba na ufunuo kamili zaidi wa mpango wa wokovu, ambao, bila shaka, ulikuwa kwa ajili ya wanadamu wote, po pote, na si tu kwa watoto wa Ibrahimu.

Kwa maneno mengine, hata kama visa vinavyohusu familia hii vinavutia, uzao wa Ibrahimu, na masomo yo yote ya kiroho tunayoweza kujifunza kutokana nayo—simulizi hizi ziko katika neno la Mungu kwa sababu ni sehemu ya historia ya wokovu; ni sehemu ya mpango wa Mungu wa kuleta ukombozi kwa watu wengi iwezekanavyo katika sayari iliyoanguka.

“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, ‘Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka’ ” (Rum. 10:12, 13). Paulo anasema nini hapa kinachoonesha kuwa injili ni kwa ajili ya ulimwengu wote? Muhimu zaidi, maneno haya yanatuambia nini kuhusiana na kile ambacho sisi kama kanisa tunapaswa kufanya ili kusaidia kuitangaza injili?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Categories:

4 comments:

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA