Sabato Mchana
Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili: Mwa. 15:6, Hes. 14:11, 1 Kor. 3:1–9, Dan. 6:1–3, Neh. 2:1–9, Kum. 4:1–9, Mdo. 2:42–47
Fungu la Kukariri: “‘Lakini habari zake zikazidi kuenea,
wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.’”
(Luka 5: 15).
Kwa miaka kadhaa, Kanisa la Waadventista Wasabato katika
eneo Fulani lilikuwa likitoa kifungua kinywa kwa muda wa siku tano kwa
juma katika shule ya awali ya eneo lile.
Ingawa serikali ya nchi ile
haikuwa ya kidini, lakini ilipitisha sheria kutoa pesa kwa kila shule ya
serikali ili kuwa na mchungaji, shule pamoja na jamii walilitaka kanisa
la Waadventista kutoa mwalimu na Mchungaji mmoja, ni nadra sana
kuliomba dhehebu moja tu kufanya hivyo. Jukumu la Mchungaji ni
kuwasaidia wanafunzi na jamii nzima ya hapo shuleni, mahitaji ya
kimwili, Kihisia, na kiroho. Fursa hii ilikua yakushangaza.
“ Nina furahia uhusiano wa kipekee na maalumu tulionao na
kanisa lako,” Mkuu wa shule alimwambia Mchungaji ambaye alikuwa
akiitembelea shule, “ Natamani madhehebu mengine, yafanye kama
unavyofanya.” Wakati Mchungaji alipokuwa anaondoka katika jamii ile,
Afisa Uhusiano wa shule ile alimshukuru kwa kile kanisa lilichokua
likifanya na kumuomba kama angeweza kuhudhuria Sabato moja.
Juma hili tutachunguza suala la kuishinda Imani ya watu ambao sisi tunahitaji kuwahudumia na kuwaleta kwa Kristo.
Somo la juma hili limetafsiriwa na Naetwe E.Kimweri pamoja na Agape P. Mrindoko.****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***



0 comments:
Post a Comment