Makanisa ni makundi yanayojitolea kwa sehemu kubwa,
yanayofanya kazi katika bajeti finyu.Mtaji wa kijamii husaidia husaidia
makanisa mahaliakuongeza nafasi ya kuyafikia malengo yake muhimu.
Utamaduni wa kale katika baadhi ya nchi huwasaidia wakulima wengine
kuleta mavuno yao ni mfano wa mtaji wa kijamii. Hii ni kwamba ingawa
inatupasa kuangalia kila hali kwa jinsi yake, lakini pale inapowezekana
ni busara kufanya hivyo, tunaweza kushirikiana na wengine ilikuyafikia
malengo yetu.
Soma Nehemia 2:1-9.Ni nini iliyokuwa matokeo ya matumani kutoka mbinguni aliyokuwa nayo mfalme Artashasta juu ya Nehemia?
Fedha ambazo alikuwa amepungukiwa (Nehemia) aliomba kwa
wenye uwezo wakampatia. Bado Bwana yupo tayari kugusa mioyo ya wale
wanao miliki maliza zake kwasababu ya kuendeleza njia ya ukweli. Wale
wanaomtumikia Bwana katika kazi zake wanapaswa kupokea msaada ambao
anawasukuma watu wake kutoa…Wenye kutoa misaada wanaweza wasiwe na Imani
kwa Kristo wala kufahamu maneno yake; lakini michango yao isikataliwe
kwasababu hiyo. “Ellen G.White, Prophets and Kings, uk.634.
Huvutia kiasi gani kwamba katika jambo hili Mungu aligusa
mioyo ya wapagani ili kuendeleza kazi yake.Hili linapaswa kutufundisha
jambo la muhimu sana hapa. Kwa viwango vyovyote vile tunavyoweza kufikia
ni lazima tuwe tayarin kufanya kazi pamoja na watu wengine,hata wale
wasio na Imani yetu au wasio na Imani kabisa, Kama kwa kufanya hivyo
tutaiendeleza kazi ya Kristo kusonga mbele Zaidi. Ingawa kwa hakika
tunapaswa kuwa makini katika ushirikiano tunaouanzisha na watu wengine.
Kwa uangalifu na kwa njia ya maombi mengi tunaweza kuifanya kazi na
wengine ambao michango yao yaweza kuisaidia kazi ile tunayo hitaji
kuifanya kwa ajili ya ustawi wa jumuiya yote. Mara kadhaa serikali, hata
mashirika binafsi na wafanyabiashara binafsi, wanapovutia na kazi zetu
za kujali wengine, watatupatia msaada wao, Msaada huu haupaswi
kukataliwa moja kwa moja au kukubaliwa moja kwa moja bila kufikiri.
Badala yake, utazamwe kwa maombi na misingi ya vipengele tofauti
tofauti, na kwa nyenzo mbali mbali na ushauri wa kutosha kabla ya
kufanya maamuzi.
Ni njia zipi unazoweza kujenga “mtaji wa kijamii”katika
jamii yako ambao waweza kuleta matokeo chanya, bali sio mafanikio yako
bali mafanikio kwa wengine?****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment