Kanisa mojawapo la waadventista wasabato katika nchi za
Afrika linakua kwa kasi. Nini siri yao? Viongozi wa kanisa walisema
kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya ukuaji huu na kutokua ubinafsi na
huduma zisizo na masharti za washiriki wa kanisa lile kwa jamii inayo
wazunguka na taifa kwa ujumla. Kujiamini kwa kanisa hili kuliko enea
nchi nzima kulichukua umakini wa rais wanchi hiyo. Alihudhuria mkutano
mkubwa wa hadhara ulioendeshwa na kanisa hilo la waadventista wasabato
aliwashukuru washiriki wakanisa lile kila mmoja kwa huduma yake.
Wakati huo huo kama wawakilishi wa Kristo tunapaswa
kutembea katika njia nyembamba. Tunahitajika, kama Yesu alivyo fanya,
kuishinda Imani na kujiamini kwao. Lakini Imani na rtumaini lao kwetu
linapaswa kupelekwa moja kwamoja kwa Kristo. Sisi ni mifereji tu.
Wanamwona Kristo kupitia sisi kwa kutokua wabinafsi, kuwa na upendo,
wenye kujali, kujinyima kwa manufaa ya watu wengine na wawe wana vutwa
kwetu kama siku zote wafanyavyo wanapo tutazama sisi kwa makini,
kwasababu sisi sote tu wadhambi, wanaweza wasipendezwe na yale yote
wanayo yaona kwetu.
Hivyo ni lazima sikuzote tuwaelekeze kwa Yesu,
katika yeye pekee wanaweza wakaweka tumaini lao pekee. Sisi wengine
mapema au baadae twaweza kuwakatisha tamaa.
Soma 1 Wakorintho 3:1-9,1 Wakorintho 5:1.Paulo
anashughulikia nini katika kanisa hili?Ni aina gani ya ushuhuda
ingeonekana hapa kama watu hawa wangekuwa wamewaalika wengine katika
kanisa lao na kuona kile ambacho Paulo alikizungumza?
Kwa hakika hatuwezi kuwa wakamilifu, au kuwa na kanisa
kamilifu kabla ya kutafuta kuwahudumia wengine. Na wakati huo
huo,tunapaswa kutafuta kuwa watu wa aina Fulani ambao ni waaminifu na
wengine waweze kujifunza kupitia sisi. Na tutaweza kufanya hivyo tu kwa
kuwa waaminifu na wenye kuwajali wengine kama Yesu alivyofanya.Kwa
hakika hapana shaka kwamba ugomvi na mapambano ndani ya kanisa
yangetokomea kama washiriki wangelenga juu ya kuihudumia jamii na
kuufunua kwao upendo wa Kristo.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment