Friday, February 27, 2015

estaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kipaji cha mtoto huanza kuonekana taratibu wakati anaendelea kukua, mara nyingi wazazi huwa wanakua wa kwanza zazi ndio wakati wa kutambua mwanaye anataka nini kwa maisha yake ya baadaye lakini kipaji cha mtoto Esther Okade kimekua cha ajabu na kumshangaza kila mmoja.
Unaweza usiamini lakini huu ni ukweli, Esther ambaye ana umri wa miaka 10 amejiunga na masomo ya chuo kikuu huria cha Uingereza miezi mitatu iliyopita akisomea shahada ya hesabu.
Eshte
Mtoto huyo ambaye anatokea katika mji wa Walsaw uliopo Midlands, Uingereza sio mtoto pekee mwenye kipaji cha aina yake, mdogo wake wa kiume mwenye miaka sita anasoma masomo ya kidato cha tano katika mchepuo wa hesabu.
MOM

Esther akiwa na mama yake mzazi, Ife
Pamoja na Esther kudahiliwa miezi mitatu iliyopita ameonekana kufanya vizuri kuzidi wenzake darasani.
Mama yake Esther aitwaye Ife anasema kitendo cha mwanae kujiunga chuo kikuu kilikuwa la kushangaza kutokana na umri wake kuwa mdogo lakini mwenyewe alijiamini na kuona anaweza.
YOUNG

Esther akiwa na mdogo wake Isaya
“Tangu akiwa na miaka saba alikuwa na shauku ya kujiunga na chuo kikuu ili atimize ndoto zake, alikua na kipaji cha aina yake darasani na baada ya miaka mitatu aliuliza tena ikabidi tumpeleke ili kuona kama kweli atamudu“– amenukuliwa Ife, mama wa Esther.
Historia inaonyesha kuwa Esther si wa kwanza kujiunga na chuo kikuu akiwa na umri mdogo, mwaka 1981 mtoto aitwaye Ruth Lawrance alijiunga na chuo kikuu cha Oxford na kuhitimu mwaka 1985.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA