Saturday, July 06, 2013

Ni sabato njema ambapo wana na binti za MUNGU walianza vipindi vya siku ya sabato kwa kuimba nyimbo za kitabuni na kujifunza masomo ya biblia,kiongozi alisimama kusisitiza juu ya kuchangia TELEVISHENI YA MORNING STAR kwa awamu ya pili, ambapo awamu ya kwanza ilikwisha fanyika mapema mwezi wa TATU mwaka,2013. Kanisa la Tandale linaundwa na kwaya ya MBIU ambayo hivi karibu ilifanya uzinduzi wa DVD namba mbili katika ukumbi wa DELUX, uliopo SINZA jijini DAR ES SALAAM.
Sabato ya leo ilikuwa maalum kwa ajili ya meza ya bwana,wana na binti za MUNGU walijumuika pamoja kwaajili ya huduma hii ambayo ni ukumbusho wa TUKIO LA MWISHO aillolifanya YESU KWA WANAFUNZI wake kama alama ya ukumbusho wa MWILI na DAMU yake kwa kula MKATE NA DIVAI ISIYOCHACHWA ..Huduma hii ilifanywa na MCHUNGAJI WA MTAA DAVID MBAGA..


SAUTI YA NNE (BASS), walio mkono wa kulia wakiimba wakati wa ibada kuu.


waimbaji wa MBIU KWAYA, wakihudumu wimbo wa kumkaribisha mhudumu wa ibada kuu.


washiri wa kasisa la TANDALE wakiwa katika ibada kuu.

 

washiriki wa kanisa la TANDALE, wakiwa katika kipindi cha ibada kuu.


vijana wa kanisa la TANDALE wakiwa makini kabisa wakisikiliza ujumbe katika kipindi cha ibada kuu.

GWIRISHA MJEMA mwimba wa sauti ya PILI kikundi cha VEGA-CAPPELA SINGERS, akiwa katika huduma ya meza ya bwana katika kanisa la TANDALE.


FRANK REUBEN LUSHIBA, mwimbaji wa sauti ya NNE kikundi cha  VEGA-CAPPELA akiwa katika huduma ya meza ya  BWANA katika kanisa la TANDALE.


Washiri wa kanisa TANDALE wakiwa katika huduma ya meza ya bwana .


Washiriki wa kanisa la TANDALE wakiwa katika huduma ya meza ya bwana


Washiriki wakiwa katika huduma ya meza ya bwana

Waimbaji wa kwaya ya MBIU sauti  ya kwanza, kanisa la  TANDALE, wakiimba kumkarisha mhudumu  wa  ibada  KUU.



Waimbaji wa MBIU  kwaya sauti ya pili kanisa la  TANDALE.

Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA