Saturday, September 20, 2014

Vikundi cha vijana Waadventista Wasabato toka Kanisa la Ilala SDA Dar Es Salaam tangu tarehe14/9/2014 hadi 28/9/2014 wapo kwa kusudi la injili katika maeneo ya Mlimba nje kidogo ya mji kasoro bahari,Morogoro.
Peter Joseph mmoja wa vijana walio katika msafara huu alisema na blog hii kuwa,timu ya uinjilisti ilianza safari yake kwa njia ya treni toka Dar Es Salaam na kuwasili kwa furaha na kupokelewa na wenyeji vizuri na mara kuanza kazi ya kuandaa mahala pa kufanyia mahubiri haya katika kijiji hiki cha Mlimba.
Mahubiri haya yanaenda sambamba na ualikaji wa watu kwa vijana nwa Holy Reunion kushirikiana na Washiriki wa kanisa la Mlimba sda kwenda nyumba kwa nyumba na kufanya huduma ya kualika watu  na kufungua madarasa ya kufundisha maandiko matakatifu na hadi jumatano kulikuwa tayari na madarasa sita na waalikaji wakiwa katika vikosi vya watu wawili wawili hadi watatu.
Ikiwa ni efoti ya wiki mbili,Sabato ya leo itakuwa tayari imekamilika wiki moja ya mahubiri haya kukiwa na wahudumu mbalimbali kama vile;-Yared Omolo-Mhubiri,Happy Ngeki&Elithabeth Richard- Afya,Japheth Chamriho-Kaya na Familia kukiwa na kwaya mbalimbali kama vile Holy Reunion,Mlimba Youth Choir na Mlimba SDA Choir..
Wiwa kuombea kazi ya Mungu MLIMBA
SAFARI IKIANZIA HAPA DAR ES  SALAAM 
WALIOSIMAMA KUSHOTO NI YARED OMOLO NA CHAMKALI NA KUSHOTO ALIYEKAA NI SAMWELI MUHAZINI

SAFARI IKIANZIA HAPA DAR ES  SALAAM 

KUTOKA KUSHOTO NI CHAMKALI,PETER JOSEPH,YARED OMOLO NA SAMWEL MUHAZINI VIJANA KATI YA WANATIMU WA EFOTI TOKA DAR

SAMWEL MUHAZINI
UJENZI UKIENDELEA KWA KUKUSANYA MBAO ZA KUJENGEA KIBWETA
KUSHOTO NI RUTH CHAURO,HAPPY NGEKI,SAMWEL MUHAZINI NA MWENYE BAISKELI NI YARED OMOLO
UJENZI UKIENDELEA
UJENZI UKIENDELEA
WADAU WAKIWA WAMEPUMZIKA BAADA YA MAJUKUM

KUTOKA KUSHOTO NI CHAMKALI,PETER JOSEPH,YARED OMOLO NA SAMWEL MUHAZINI VIJANA KATI YA WANATIMU WA EFOTI TOKA DAR
NDANI YA USAFIRI KUELEKEA MLIMBA MOROGORO
YARED OMOLO NDANI YA TRENI KUELEKEA MLIMBA
NDANI YA USAFIRI KUELEKEA MLIMBA MOROGORO

HABARI NA PETER JOSEPH
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA