Sabato ya tarehe 25/10/2014 ilikuwa ni ya pekee na furaha sana kwa kanisa la Shangani na Mtwara kwa ajili ya wana na binti za Mungu waliojitoa kwa kusikiliza ujumbe wa wokovu kupitia redio Info iliyopo Mtwara inayomilikiwa na mshiriki wa kanisa la Mtwara. Wabatizwa hawa kati yao 8 walitoka kijiji cha "IMEKUWA" HAWA NDIO WALIPOKEA INJILI KWA NJIA YA REDIO NA KUANZA KULITAFUTA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO. Hata hivyo katika kijiji hicho bado wapo wengine waliojitoa baada ya kuona wenzao wamebatizwa, Hitaji kubwa la waumini hawa kwa sasa ni kuwa na mahali pa kuabudia kwa kuwa katika kijiji hiki hakuna kanisa, Ninapenda kuwaalika tusaidiane katika kujenga kanisa la IMEKUWA. Pamoja na ubatizo wa hao walikuwepo wengine walitokea kanisa la Shangani na mmoja wao alitokea kanisa la Mtwara huyo (MCHINA). JUMLA WALIKUWA 13. Jina la Bwana liinuliwe kwa matendo yake ya ajabu. Taarifa imeletwa na Mchungaji wa Mtwara Pr. Zetti Ndola
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***






0 comments:
Post a Comment