Wednesday, October 29, 2014

Source: MORNING STAR TV - BIG DAY.
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano
Southern Highlands Conference
P.O.Box 99 Mbeya

09/10/2014
Wachungaji wa Mitaa, Wazee wa Kanisa,
na Waamini Wote
Southern Highlands Conference
Wana na Binti za Mungu,
YAH: TAREHE 01/11/2014 NI SIKU MAALUM YA KUOMBEA NA KUCHANGIA MORNING STAR TV.
Ndugu wasafiri wenzangu wa kwenda Mbinguni, nawasalimu katika jina la BWANA wetu Yesu kristo.
Kichwa cha habari cha husika.
Kwanza kabisa napenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru wote kwa sadaka mliyoitoa wakati wa siku ya Uzinduzi wa Morning Star TV Tarehe 19/04/2014 ambayo kwa conference yetu tulipewa goli la million 40 nasi tuka toa takribani million 8 tukawa na upunguifu wa milioni 32. Kutokana na Kutofikiwa kwa goli letu japo sio sisi peke yetu ambao hatukufikia goli Uongozi wa Morning Star TV Kwa kushirikiana na Uongozi Wa Union zote mbili yaani STUM na NTUC Wameona ili kuwezesha TV yetu Ambayo tayari Ipo hewani kwa majaribio kudumu Kutangaza Ujumbe wa malaika wa tatu kunasababu ya kukamilisha mambo yaliyo salia ili kupe wa Ruhusa ya moja kwa moja kuendelea kutangaza habari njema. Pesa iliyo kusudiwa kukusanywa kwa Tanzania nzima ili kukamilisha na kuanza TV yetu ni Million 500. Pesa iliyo kusanywa na kutumika hadi sasa ni Million 287,350,000 Upungufu ni Million 225.
Million 225 Zinazo hitajika kutolewa tarehe 01/11/2014 ni kwaajili ya mambo yafuatayo:
1. Garama za urushaji matangazo kwa miezi 6
a. BTL (King’amuzi cha Digtec ) ni 20.4m”(Kinaonekana Daresalaam, Dodoma, Mwanza, Na Arusha)
b. AGAPE (King’amuzi cha TING) ni Million 105,200,000( Kinaonesha Mikoa yote iliyo baki na pia Kinaonesha katika Nchi 11 za Afrika)
2. VIFAA VYA KURUSHA MATANGAZO moja kwa moja (LIVE) ni Million 36,500,000
3. GARI LA UZALISHAJI vipindi ni Million 25,500,000
4. LESENI-17,000,000
5. DHAMANA YA MIKATABA URUSHAJI 20,400,000
Muhimu: Hebu Wachungaji na wazee wa kanisa tutoe wito kuwa tafuta Marafiki wa Morning Star TV ambao watakuwa tayari kuchangia kiasi watakacho panga kila mwezi. Watu hawa watapewa kadi maalum za kujisajiri na marafiki wa Morning Star TV ambazo zime ambatanishwa.
Pia kila kanisa lipewe Bango moja Linalo tangaza juu ya Siku hii.
Yafuatayo ni Magoli ya Kila Mtaa Na Wachungaji Mtagawa kwa kila kanisa na hatimaye kanisa litagawa kwa kila mshiriki:



****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA