Sunday, November 02, 2014

Mchungaji Charles S.Mndambi akizungumza wakatika wa ibada katika kanisa la Waadventista Wasabato Kimara hapo jana.
Mchungaji Charles Mndambi toka mitaa miwili ya Kigamboni na Kibada amekuwa sehemu ya mbaraka katika uchangiaji wa Televisheni ya Morning Star katika kanisa la Waadventista Wasabato Kimara.Somo la ufunguzi akilijenga katika picha ya kwamba,Ufunuo 14:6"Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa," hii huonesha wazi juu ya fundisho la ujumbe ulibebwa na runinga ambayo ni yenye kuleta tumaini lililo ndani ya Kristo Yesu mwenyewe na hvyo ili kuondoa mazingira ya shetani aliyoyaweka juu ya anga hili hasa kwenye sateliti kwa picha chafu na video yanipasa mimi na wewe kushiriki kikamilifu kuchangia na kuombea changizo hili.
Mpaka kufungwa kwa vipindi vya Sabato hapo jana,changizo lilikuwa limefikiwa kupatikana,yaani goli la kiasi cha 1,132,200/= toka kwa washiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kimara.
OMBEA NA CHANGIA MORNING STAR TELEVISHENI SASA..


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA