HABARI NA mwananchi.co.tz
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Mpendwa msomaji nakushukuru kwa kutenga muda wako kwa ajili ya
kusoma safu hii. Katika makala yetu ya leo nitaendelea kutoa maelezo ya
namna bora ya kutumia dawa za kutibu U.T.I. Kwa faida ya wasomaji wapya
nitaelezeza tena kwa ufupi kuhusu ugonjwa wa U.T.I.
U.T.I ni kifupi cha (Urinary tract Infection) ni
ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo. Ugonjwa huu husababisha maumivu makali
mwilini. Baadhi ya dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mwili kuwa
dhaifu, kujisikia kichefuchefu mara kwa mara, mkojo kuwa wa moto na
mchafu, maumivu wakati wa kukojoa, maumivu kwenye kiuno na tumbo kuuma.
Ugonjwa huu hutokea pale mlango wa njia ya haja
ndogo inaposhambuliwa na bacteria. Bakteria hawa wasipotibiwa mapema
huenea hadi kwenye figo na athari zake zinaweza kuwa mbaya zaidi.
Uganjwa huu hutibika kwa dawa nyingi jamii ya
vijiua sumu (antibiotic). Baadhi ya dawa hizi ni tetracycline,
ampicillin, Ciprofloxacin, Cefalexin, Cefadroxil, clavam, Fosfomycin,
Monurol, Furadantin, Sulfam ethoxazole, co-trimax, ampicillin,
gentamicinn na nyinginezo.
Wiki iliyopita nilieleza namna ya kutumia dawa
tetracycline katika kutibu U.T.I. Katika makala yetu ya leo nitaeleza
nammna ya kutumia ampicillin kutibu U.T.I. Ampicillin ni moja ya dawa
jamii ya vijiuasumu (antibiotics) inayotumika kutibu magonjwa
yanayoambukizwa na bakteria ikiwemo U.T.I. Dawa hii hutibu U.T.I kwa
kuingilia ukuaji wa bakteria walioko mwilini kwa kuua seli zake wakati
wanakuwa. Hali hii husababisha seli za bakteria kuwa dhaifu, hatimaye
kufa.
Ampicillin ni jina la jumla la dawa hii na
imesajiliwa. Inatumika Tanzania kwa majina tofauti ya kibiashara. Baadhi
ya majina haya ni Omnipen, Polycillin na Principen.
Taarifa muhimu kabla ya kutumia ampicillin:
Baada ya kufanyiwa vipimo na kubainika kuwa una
U.T.I unatakiwa kujadiliana na daktari kuhusu dawa atakazokupatia. Kuwa
huru na muwazi kumweleza daktari kuhusu mstakabali wa afya yako.
Mweleze daktari au mfamsia au muuguzi kama una
ujauzizo au unapanga kupata ujauzito wakati ukitumia ampicilini au
unanyonyesha. Baadhi ya dawa katika kundi la vijiuasumu haziruhusiwi kwa
kuwa zinaweza kuwa na madhara kwa mtoto aliyeko tumboni. Hata hivyo
ampicillin inaweza kutumia. Kumbuka kutokutomia dawa pasipo maelekezo ya
daktari hasa wakati wa ujamzito au kunyonyesha. Pia mweleze daktari,
mfamasia au muuguzi kama unatumia dawa nyingine za tiba au vyakula
nyongeza (food supplement), huwa unapata mzio ukitumia baadhi ya dawa au
vyakula na una matatizo ya tumbo au kuharisha. Taarifa hizi
zitakusaidia wewe kuandikiwa dawa zitakazokufaa kulingana na hali yako
ya kiafya.
================
================
Baadhi ya dawa za tiba haziwezi kufanya kazi
sanjari na dawa nyingine. Ampicillin pia zina tabia hii. Mweleze daktari
kama unatumia dawa yoyote kabla hajakuandikia dawa. Baadhi ya dawa
ambazo hazitumiwi sanjari na ampicillini ni tetracycline hasa doxycline.
Dawa hii huingilia utendaji kazi wa ampicillin mwilini na kuifanya
kukosa ufanisi. Dawa nyingine ambazo hazipaswi kutumika sambamba na
ampicillin ni Probenecid, Allopurinol, Anticoagulants (heparin,
warfarin) au methotrexate na Aminoglycosides (mfano; gentamicin.
Probenecid huongeza madhara kwa mgonjwa kama tutakavyoona baadaye na
Allopurinol inaweza kuongeza vipele kwenye mwili.
======================
======================
Kwa upande wa Anticoagulants hasa heparin,
warfarin au methotrexate, haishauriwi kwa kuwa ampicillin inaweza
kumwongezea madhara mgonjwa. Haya ni madhara ambayo kila anayetumia dawa
huyapata na yanavumilika.
Dawa za Aminoglycosides hasa gentamicin na za
kupanga uzazi hazitumiki sanjari na ampicillin kwa kuwa zinaweza
kupunguzwa nguvu ya utendaji kazi wake mwilini.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***




0 comments:
Post a Comment