DARUBINI YA IMANI
Pr Dominic
Mapima.
Somo - Mahubiri ya hadhara
– Morogoro.
HOTELI YA MUNGU DUNIANI
UTANGULIZI
KATIKA DUNIA YETU TUMEONA NA KUTEMBELEA HOTELI
MBALIMBALI,HOTELI HIZO ZIMESHEHENI AINA MBALIMBALI ZA VYAKULA NA VINYWAJI
VINAVYOONEKANA NI VYEMA NA KUPENDWA NA WATU. KATIKA SOMO HILI TUTAANGALIA JUU
YA HOTELI NYINGINE LAKINI JAMBO LA KUSHANGAZA NI KUWA HII SASA NI HOTELI YA
MUNGU DUNIANI.
KWANINI
HOTELI YA MUNGU?
WAKATI FULANI HOTELI HIZI ZINAZOONGOZWA NA WATU WA
DUNIA ZIMEZAA MATOKEO MABAYA KWA WATEJA, MATOKEO AMBAYO YAMEWAPA MAJUTO MAKUBWA
NA KULAUMU NIA YAO NJEMA YA KUTAFUTA HUDUMA KATIKA HOTELI HIZO, HIVYO KWA HALI
HII NI MUNGU PEKEE ANAWEZA KUWA DIRA KWA WANADAMU KWA KUWAPA KANUNI BORA NA
VIWANGO KATIKA SWALA ZIMA LA ULAJI.
KISA:-
Watu fulani walikuwa wakisafiri kuelekea mikoa ya
kusini’ muda wa chakula cha mchana ulipofika gari ilipaki na wakaingia kwenye
vibanda vya hoteli ndogondogo vilivyokuwa njiani hapo, wakiwa wameketi tayari
kwa kula waliagiza supu, pindi wakiendelea kunywa ndipo mmoja wa wateja hao
alisikika akiomba kuongeweza nyama!_ghafla alisikia sauti ikijibu toka jikoni
na kusema’ “Samahani kaka kaumbwa kenyewe tulikokachinja leo kalikuwa
kadogo!!!!!!!!!_ wale wateja walianza kutapika!!!!!!
Tunapozunguzia Hoteli tunazungumzia jengo lililobuniwa
na mwanadamu kwaajili ya kutoa huduma ya vyakula, hivyo tunapozungumzia hoteli
ya Mungu duniani maana yake ni jengo la Mungu ambamo pia uhusika na ulaji,
maandiko matakatifu ya Biblia yanaweka bayana juu ya jengo hilo la
Mungu(hoteli)hapa duniani ambamo humo ni vyakula vyenye ubora tu hupaswa
kuingizwa na ni kwa kadri ya maelekezo ya mmiliki wa hoteli hiyo, hebu tuone
hoteli hiyo na maelekezo yake ya vyakula vinavyopaswa kuingia humo.
Hoteli ya
Mungu ni ipi?
Bilblia
inaanza kwa kusema:-
1Wakoritho 3:9
Maana
si tu wafanyakazi pamoja na Mungu, ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Biblia katika fungu
hilo inamtaja mwanadamu kuwa ni shamba la Mungu na pia ni jengo la Mungu, hivyo
kimsingi mwili huo wa mwanadamu (jengo) ndiyo hoteli ya Mungu duniani katika
farsafa ya kiroho, tamko la Yesu akiwa mbinguni kupitia kinywa cha Yohana
inapigia mstari farsafa hiyo ya kiroho.
Ufunuo 3:20
Tazama,
nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kufungua mlango,
nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, nayeye pamoja nami.
Tamko hilo la Yesu
linabeba dhana nzima ya kimahusiano ya kila nyanja anayokuwa nayo Mungu na mtu
aliyeamua kumpokea kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake, neno alilotumia Yesu
hapo ni kuwa “mtu akifungua mlango
ataingia kwake naye atakula pamoja naye”.
Neno hilo kula
pamoja naye pamoja na kuwa lina tafsiri pana sana na ya nyanja nyingi lakini
pia inahusika na ulaji wa kawaida kwa kuwa kiukweli katika mafungu mengine
Biblia inataja kanuni za kimsingi za ulaji unaokubaliwa na Mungu ambao mtu
akiufuata na kuenenda kwa huo basi bilashaka huko ndiko kula pamoja na Mungu.
(yaani kula kwa kufuata mapenzi na Baraka za Mungu).
Hivyo Mungu hula
pamoja nasi kwa njia ya kudhinisha na kubariki tulacho.
1Wakoritho
6:17 Lakini
yeye aliyeungwa na Bwana ni roho naye.
Mtume Paulo anaweka
mkazo dhana hiyo ya Mungu kujihusha na kila nyanja ya mwanadamu, kwa kusema
kuwa sisis tu roho mmoja na Bwana.
Na ndipo baada ya
tamko hilo ndipo tena mtume Paulo anafunuliwa kuandika kile kinachobainisha
wazi ukweli wa vile Mungu anavyojihusisha na hata na ulaji wetu, na jinsi
tunavyopaswa kusikiliza maelekezo yake katika swala la ulaji ili tumtukuze pia
hata katika swala la ulaji kwa kuitendea haki hoteli yake yaani miili yetu.
1Wakoritho
10:31
Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno
lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
JE
KULA KWA UTUKUFU WA BWANA NI KWA NAMNA GANI?
Yako mambo makuu mawili yanayoweza kutajwa kuwa
ndiyo kula kwa utukufu wa Mungu ambayo ni:-
-
Kufuata
maelekezo ya kanuni ya ulaji na aina ya vyakula vilivyoruhusiwa na Mungu
mwenyewe kuingia katika miili yetu (hoteli yake).
-
Kwakuwa tu roho
mmoja na Bwana tusingepaswa kula kwa namna ambayo itakimbiza uwepo wake au
kuharibu utukufu wake maishani mwetu.
Kufuatia maelekezo
hayo hasa hayo ya kwanza yahusuyo kula kwa utukufu wa Mungu, bilashaka wali
linaloibuka hapo ni kuwa je’ basi! Mungu alitoa maelekezo juu ya vile
vinavyopaswa kutumika kama vyakula kwa watu wake?
Kumbuka
Mungu alisema”
Zaburi
84:11..sitawanyima
kilicho chema hao waendao kwa ukamilifu…..
Hivyo Mungu mwenye
aliahidi kuwapa wanadamu vyakula vilivyo bora ambavyo kimsingi ndivyo
vinavyompendeza yeye mwenyewe pia.
MUNGU
ALIPOANZA KUAINISHA CHAKULA NA VISIVYO VYAKULA.
Kama hatua ya
kutimiza ahadi yake ya kumpa kilichochema mwanadamu aendae kwa ukamilifu, Mungu
kupitia mzee Nuhu’ alianza kuainisha vilivyo visafi na visivyo visafi.
Jambo la msingi la
kuelewa ni kuwa hayo yalifanyika kabla ya kunza taifa la Wayahudi (Israel)
kwahiyo yalikuwa ni maelekezo yaliyohusu afya ya mwanadamu yeyote na siyo
tabaka Fulani la umma./ hebu tusome:-
Mwanzo
7:1-2
Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe katika
safina; kwamaana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
(2) Katika wanyama wote waliosafi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika
wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke.
Maelezo ya Mungu
kwa Nuhu katika andiko hilo yanaweka wazi juu ya vile Mungu mwenyewe aliyeumba
namna alivyoweka makusudi yake kwa kila mnyama aliyemuumba, hapo alimaanisha
wazi kuwa Nuhu asingepaswa kuwaona wanyama wote katika uwiyano, badala yake
kati ya hao wako waliosafi na wasiyo safi na kwa maana nyingine basi hata
makusudi ya kimatumizi ya wanyama hao ni tofauti.
Kumbuka
killakitu kilichoumbwa kina makusudi yake’
Mfano:
Leo hii wako watu ambao wanakata kope(nywele
za juu ya jicho) zao kwa hisia kwamba hazina kazi, lakini kimsingi kope hizo
ziliwekwa ili kuzuia maji yenye sumu toka kichwani yanapotelemka kutokea
utosini yasiingie moja kwa moja jichoni, badala yake yasukumwe pembeni na kope
hizo.
Hivyo kwajumla
matumizi ya wanyama hao hayafanani, na ndipo basi tunaposoma Biblia Mungu hapo
mbeleni kipindi cha wana wa Israeli aliainisha wanyama hao wazi, yaani wale
wanaoliwa na wale wasiyoliwa pamoja na ndege samaki nk.
Lawi
11:1,2,3,4,6,7,8
Bwana akanena na Musa na Haruni ,na
kuwaambia, (2) Neneni na wana wa Israeli , mkiwaambia, Wanyama hawa ndiyo wenye
uhai mtakaowala, katika hayawani wote waliyo juu ya nchi. (3) Kila mnyama
mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua,
katika hayawani, hao ndiyo mtakaowala (4) Pamoja na hayo, wanyama hawa
hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia
kwakuwa yu acheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. (6) Na sungura,
kwasababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.(7) Na nguruwe,
kwasababu yeye anazo kwato, nimwenye miguu iliyopasuka kati , lakini hacheui,
yeye ni najisi kwenu, (8) Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao
ni najisi kwenu.
Hao ndiyo wanyama
waliotajwa kwa uwazi kuwa Mungu hakukusudia wawe chakula, kumbuka wakatika ule
wa Nuhu tena kabla ya taifa la Wayahudi kuanza Mungu alishaweka bayana juu ya
tofauti ya wanyama hao, yaani wako waliyosafi na waisiyo safi.
Lakini pia jambo la
kukumbuka ni kuwa wale wasiyo safi waliwekwa ka idadi pungufu ikiwa ni
kiashiria kwamba matumizi yao hayakulenga chakula, tendo ambalo Bwana Yesu pia
alilidhihidhirisha kama tutakavyoona hapo mbele kidigo.
Kwa habari ya
samaki Biblia imeainisha kuwa wale wanaopaswa kuliwa ni wale wenye magamba na
mapezi pekee, na ndege pia wametajwa kama unavyoweza kujisomea katika sura hiyo
hiyo ya kitabu cha Walami 11:13-20.
JE
YESU ALIPOKUJA ALIBADILI KANUNI HIYO YA ULAJI?
Ni jambo
linaloshangaza kulisikia toka kwa wachungaji na waalimu mbalimbali wa dini
katika madhehebu ya Kikristo, wakidai kuwa ati hiyo ilikuwa ni sheria ya mpito
tu na ilihusika na wana wa Israeli pekee na hivyo kwasasa baada ya neema ya
Kristo tunaweza kula chochote na hata hivyo vilivyoharamishwa na siyo dhambi.!
Kile kinachoonekana
kuwa ndicho kigezo cha tafsiri hiyo yenye utata, ni tendo la Yesu kuatamka kuwa
kile kimwingiacho mtu akiwezi kumtia unajisi.
Marko
7:14 kimwingiacho mtu akimtii unajisi…….
Kupitia kisa hicho
cha andiko hilo ndipo changamoto ilipoanzia.
Uchunguzi
wa kisa hicho.
Ni jambo la msingi kueleweka kuwa kisa hicho
kimechukuliwa vibaya na baadhi ya wasomaji hao wa Biblia, na kile
kilichowapotosha watu zaidi ni kule kutozingatia kanuni katika usomaji wa
Biblia, katika kisa hiki msomaji kwanza akipaswa kuzingatia kanuni kuu mbili za
usomaji wa Biblia nazo ni:-
-
Kujua wazo (hoja) kuu jadiliwa katika andiko hilo
(discussed matter).
-
Kulinganisha kisa hicho na maandiko mengine ili
kupata wazo halisi (comparative study of the Bible ). Mhubiri 7:27… nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili ili kutafuta
jumla….
Kwa kufuata kanuni
hiyo ya kwanza ya kungalia wazo kuu jadiliwa,tunaweza sasa kusoma andiko husika
kwa kunzia aya ya kwanza ya kitabu cha Marko ili kuona chimbuko la kisa na nini
hasa hoja kuu.
Kujua wazo (hoja) kuu jadiliwa
katika andiko hilo (discussed matter).
Marko
7:1-3
Kisha Mafarisayo, na baadhi ya
wandishi waliotoka Yerusalemu, walikusanyika mbele yake. (2) Wakaona wengine
katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyo nawiwa.
(3) Maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali,
wakishika mapokeo ya wazee wao.
Mpendwa msomaji
wangu ni imani yangu kuwa hoja hii sasa aitakuwa tatizo kwako, kumbe kile
kichopelekea Bwana Yesu kutoa kauli hilo ilikuwa ni kujibu hija hii mahsusi
ambayo ilikuwa na mtazamao wa kufanya mapokeo ya wazee yasiyo neno la Mungu
kuwa ndiyo mwongozo wa maisha ya mitume wa Yesu, kama tulivyosoma kuwa kile
kilichokuwa chanzo cha hoja hiyo ni matakwa ya Wayahudi na Mafirisayo kuwaona
mitume wakinawa hadi kwenye viwiko ili kufata mapokeo hayo ya wazee wao.
Katika tukio hilo
ieleweke kuwa hapakuwa na chakula najisi kilichokuwa kikiliwa na mitume, bali
Mafarisayo walitaka kuanzisha aina yao ya unajisi inayotokana na kula bila
kunawa hadi kwenye kiwiko cha mkono, hivyo kauli ya Yesu kuwa kimwingiacho mtu
hakimtii unajisi ililenga kile kinachotokana na kula bila ya kunawa kwa
taratibu walizotaka wao na si kuwa Yesu alimaanisha vyakula ambavyo tayari
viliitwa najisi.
Kauli ya Yesu
mwenyewe alipokuwa akihitimisha tamko lake inafunga mjadala huu:-
Mathayo
15:20
Hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula
kabla hujanawa mikono hakumtii mtu unajisi.
Hitimisho hilo la
Yesu katika kisa hicho ni jibu tosha kuwa hakuwa akitoa tamko la jumla la
kuruhusu vyakula najisi badala yake hoja ilikuwa ni kula bila kunawa.
Lakini pamoja na
hayo, kama Yesu alimaanisha kuwa ni chochote kikimwingia mtu hakimtii unajisi,
basi maana yake ni kuwa hapo Yesu alikuwa akihalalisha vitu vungi ikiwemo Pombe katika aina zake ambazo hutoka
kwa njia ya mkojo, huenda sigara, bangi
nk ambavyo navyo haviingii moyoni.
-
Kulinganisha kisa hicho na maandiko mengine ili
kupata wazo halisi (comparative study of the Bible ). Mhubiri 7:27… nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili ili kutafuta
jumla….
Kanuni hiyo ya pili
iliyokiukwa na wale wanaohalalisha vilivyoharamishwa kwa kutumia mgongo wa
tamko hilo la Yesu ingeweza kuwa msaada mkubwa endapo wahusika wangekubali
kuitumia katika kutafuta ukweli wa swala hili, katika andiko hilo mhubiri
anasema “nimeyaona hayo kwa kulinganisha
hili na hili ili kutafuta jumla (Mh 7:27).
Kwa kutumia kanuni
ya kulinganisha maandiko utagundua kuwa kamwe tamko la Yesu halikulenga Kuruhusu vitu alivyovikataza kuwa visiliwe na
kuvifanya kustahili, pia ikumbukwe kuwa kuzuiwa kwa vyakula hivyo yaani baadhi
ya wanyama ndege na samaki haikuwa
adhabu kwa wanadamu bali ilkuwa ni kwa sababu za kiafya na makusudi yake ya
uumbaji wa viumbe hivyo kwamba baadhi yake aliona kuwa visingefaa kuwa chakula.
Zaburi
84:11..sitawanyima
kilicho chema hao waendao kwa ukamilifu…..
Isaya
55;14…kwani kutoa fedha kwa kisicho chakula?...
Jinsi
Yesu alivyoendelea kuainisha vyakula na visivyo vyakula.
Hili ni jambo
linalo nishangaza sana, inaniwia vigumu kuamini kuwa wachungaji na waalimu
mbalimbali katika madhehebu za Kikristo hawajawahi kulisoma andiko hili la Luka
na kujionea wenyewe tamko hili la Yesu na jinsi alivyoainisha vyakula na
visivyo vyakula yeye mwenyewe:-
Mathayo
7:9 -11
Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye mwanawe
akimuomba mkate, atampa jiwe? (10)Au akiomba samaki, atampa nyika? (11) Basi
ikiwa ninyi ,mlio waovu,mnajua kuwa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi Baba
yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wampendao?
Katika andiko hilo
kama ulivyoona Bwana Yesu anaainisha kati ya vyakula na vuisivyo vyakula,
sehemu ya kwanza aya ya 9’ anaonyesha kuwa mkate
ni chakula na jiwe si chakula na
hivyo haistahili kumpa motto jiwe. Aya ya 10’ anaonyesha tena kuwa samaki ni
chakula lakini nyoka si chakula na haistahili kumpa mototo nyoka aombapo
chakula.
Sasa kwa maelezo
hayo ya Yesu wale wanaodai kila kitu kimehalalishwa wanatumia ushahidi gani
kuthibitisha madai hayo?
KWA
UJUA HAKIKUWA CHAKULA YESU ALIANGAMIZA NGURUWE’.
Miongoni mwa mambo
ya msingi ya kujifunza kwa Yesu juu ya mpango wake wa vyakula katika hoteli
yake ni tukio hilo la kuangamiza nguruwe, ili kuelewa ujumbe wa Yesu katika
katika tukio hilo rejea kwa kutafakari matukio mbalimbali ya huruma
aliyoyafanya Yesu kwa kuwapa watu chakula kama vile:-
-
Muujiza
wa ongezeko la mikate na kulisha watu wengi.
-
Muujiza
wa ongezeko la samaki pamoja na kuwawezesha kina Petro kupata samaki baada ya
kuhangaika usiku kucha.
-
Muujiza
wa kugeuza maji kuwa divai ili kunywesha watu arusini.
Matukio hayo yote
yanaonyesha jinsi Yesu alivyokuwa na moyo wa huruma kwa watu pale ambapo
inaonekana wametindikiwa na chakula. Lakini katika tukio hili tunaona Yesu
anafanya kinyume pale alipoamuru kundi kubwa la nguruwe kuingiwa na mapepo na
kufia ziwani.
Luka
8:32-33
Basi, hapo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe
wakilisha mlimani,; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale, akawapa ruhusa. (33)
Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi likatelemkia gengeni
kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji.
Kimsingi huu
ulikuwa ni ujumbe wa kimya wa Yesu ambao kimsingi unaungana na kile tulichosoma
katika kitabu cha Mwanzo juu ya idadi ya wanyama aliotakiwa kuwaingiza katika
safina, kumbuka Mungu alimwambia wale wanyama walio safi aingize saba saba na
wasiyo safi wawili wawili, hivyo kwa muktadha wa tukio hilo la Yesu kungamiza
nguruwe tunaona mwakozi akifanya kile kile ambacho aliamuru kifanyike wakati wa
Nuhu, kumbuka wakati pia idadi ya wanyama wasiyo safi ilipaswa kupungua na hapa
sasa Yesu anaamuru kupungua kwa idadi wa wanyama hao ambao si chakula katika
mji ule wa Gerasi.
2Wakoritho
6:17-18
kwahiyo,Tokeni
kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami
nitawakaribisha.(18) Nitakuwa Baba kwenu nanyi mtakuwa kwanu wanangu wa kiume
na wakike
Tafakari upya
na fanya matengenezo juu ya ulaji ili ule vile vinavyo mpendeza Bwana.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***



0 comments:
Post a Comment