Tuesday, December 30, 2014

 SONDA YA DIHLU ni kundi linapatikana DAR ES SALAAM – TANZANIA katika kanisa la WAADVENTISTA WASABATO UKONGA.  Kundi hili linahubiri injili kwa njia ya Uimbaji wa muziki wa Injili aina ya Acapella yaani muziki uimbwao bila kutumia vyombo vya Muziki.
Jina SONDA YA DIHLU linatokana na lugha ya KISUKUMA likiwa na maana ya NYOTA YA ASUBUHI kwa Kiswahili.  Kundi hili lilianza rasmi  16/09/2006 likiwa na jumla ya waimbaji watano ( 5 ).  ISAYA DANIEL ( Lead/ Second Tenor ),  ELISHA BARNABA ( First Tenor ),  BAEL DISHON ( Baritone ),  JIMSON  MLOWE ( Second Tenor ) na  EMANUEL TUNZO ( Bass ), chini y a uongozi wake BAEL DISHON (Mwenyekiti), ISAYA DANIEL (Katibu).  


 Na mnamo mwaka 2007 Kundi lilifanikiwa kurekodi Albamu ya kwanza inayojulikana kwa jina la “HUKUMU” iliyorekodiwa “ MALAIKA RECORDING STUIDIO” na kurudiwa mwaka 2008  na “MORNING STAR FM RECORDING STUDIO”. Na mwishoni mwa mwaka 2011 kundi lilifanikiwa kurekodi albamu ya pili inayojulikana kwa jina la “HALLELUYA TUKIFIKA JUU”. Kwa sasa kundi lina jumla ya waimbaji saba ( 7), ISAYA DANIEL ( Lead/second Tenor ),  ELISHA BARNABA ( First Tenor ),  MSAFIRI TUNZO ( Baritone ),  JIMSON MLOWE ( Second Tenor ),  RICHARD YESSAYA ( Bass ),  EMMANUEL TUNZO ( Bass ), na  JACKSON FANUEL (Lead/Second Tenor), Chini ya uongozi wake ELISHA BARNABA( Mwenyekiti), JIMSON MLOWE (Katibu), na MSAFIRI TUNZO (Mhazini).  Kundi hili tangu kuanzishwa kwake  limekuwa likihudumu katika mikutano mbalimbali  kama vile  MAHAFALI ZA ASSA NA THISDASO,  MIKUTANO YA INJILI YA HADHARA (EFFORTS ), MIKUTANO YA MAKAMBI, SABATO MAALUM ZA WAGENI na MATAMASHA MBALIMBALI YA NYIMBO ZA INJILI, NDOA NA HARUSI MBALIMBALI,  PAMOJA NA HUDUMA MBALIMBALI ZA KIROHO NA KIJAMII, ndani ya nchi katika maeneo ya MOROGORO, MBEYA, ZANZIBAR, MTWARA, PWANI, DAR ES SALAAM, na nje ya Nchi kama; KAMPALA nchini UGANDA ( WORLD MUSIC-FESTIVAL)Mwaka-2010-na NAIROBI, NAKURU nchini KENYA Mwaka 2011.

DHAMIRA YAO
Kuihubiri Injili ya YESU kwa kasi na katika mazingira yeyote yale, mahali popote duniani,  mpaka YESU anaporudi mara ya pili kutuchukua kwenda mbinguni.

DIRA YAO
Kuwa kundi bora linalofikika na kuwafikia watu kwa Wepesi na urahisi zaidi popote duniani, pia kuwa na “Recording Studio” Kubwa.


0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA