Thursday, December 04, 2014

Kushoto ni bibi Nancy mke wa raisi wa wasabato ulimwenguni na Kulia ni Raisi wa  wasabato ulimwenguni ndugu,Ted NC Wilson
HABARI NA ANN(ADVENTIST NEWS NETWORK)


Rais  wa waadventista wasabato Ted NC Wilson atoa rambirambi kwa familia za wale waliouawa katika mashambulizi ya wapiganaji nchini Kenya Novemba 22. Katika shambulio hilo la watu 28 waliokua kwenye  bus  hilo miongoni mwao walikua ni waumini wa kanisa la kiadventista la wasabato, Rais  wa waadventista wasabato Ted NC Wilson alisema yafuatayo wakati anatoa  mchango wake wa Rambi rambi.
========
Kwa niaba ya ya waumini Wakisabato ulimwenguni mzima, tumesikitishwa sana na vifo vya kutisha huko nchini Kenya na ukiangalia katika shambulio hilo kuna wengine ni waumini wa kanisa hili la kisabato  Mioyo yetu imejaa majozi makubwa sana hasa  kwa familia ambazo wamepoteza wapendwa wao, wakiwemo watoto, katika mauaji ya kikatili.

Mke wangu, Nancy, na yeye  anapenda kutoa salamu za  rambirambi kwa familia za Kikristo zilizokumbwa na tatizo hilo.Hatuwezi kuelewa nikwaniani mauaji ya  kutisha yamechukua nafasi kubwa nchini Kenya . Hata hivyo, Roho Mtakatifu kama Msaidizi inaweza kuleta faraja kwetu. Mim na familia yangu nimejitolea kuwaombea familia hizi zilizo kumbwa na hili tatizo la kuondokewa na wapendwa wao.
=========
Ni baraka kujua kwamba katika siku za usoni, wakati Yesu atakaporudi, Naye atafuta kila aina ya machozi. Wafilipi 4: 7 inasema, ". Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu"
Pamoja na mauaji katika ulimwengu huu wa sasa, kuna matumaini ya baadaye wakati Kristo atarudi. Kwa uwezo wa Mungu, hebu kuwa waaminifu kwa Neno lake na kwake! Nini faraja kujua kwamba kurudi kwa Yesu Kristo ni kumekaribia na tunaweza kuhesabu tumaini la Kikristo uzima wa milele.
==========

Naomba kutoa salamu hizi za rambi rambi kwa familia zote zilizo kumbwa na tatizo hili na Mungu awe mfariji mkuu katika tatizo hili. Amen

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA