Sunday, December 21, 2014

Akizungumza na injilileo blog hapo jana katika viwanja vya kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni ,mkuu wa kamati ya maandalizi na mipango kwa safari hii ya vijana na wanafunzi wa vyuo vikuu (TUCASA) kwa kanda ya Dar Es Saam Mr.Lazack amesema maandalizi ya wanatimu yako vizuri.
Katika mkutano huu,wanachama wa Tucasa kwa kanda hii ya Dar wapatao 52 wapo njiani kuelekea Kenya katika makutano haya ambayo yataanza hapo kesho ikiwa ni siku rasmi ya kuanza mkutano huu mkubwa wa vijana ambao hufanyika kila mwaka na mwaka jana ukifanyika katika chuo cha Waadventista Wasabato Bugema nchini Uganda na mwaka huu kufanyika katika chuo cha Waadventista Wasabato Baraton Kenya.
Kwa program zilizoandaliwa na vijana wa Tucasa ni kama vile;-kukariri mafungu ya lessoni ya mwka mzima(robo nne),huduma ya kitabibu toka kwa wanafunzi madaktari wakitokea vyuo vya Imtu,Kairuki na Muhimbili na program nyingine ikiwa ni pamoja kuhesabu muda au masaa ya binadamu kiutendaji kwa jumla ya miaka yake ya kuishi,yaani kama ski za binadamu kuishi ni 70 je kwa miaka hiyo atakuwa kaoga,kafua,amekula,ametembea au amelala kwa masaa mangapi? 
Kuelekea kwenye mkutano huu,wanachama toka kanda nyingine ni kama vile;Morogoro ni wanachama 9,Dodoma ni 23,Mbeya na Iringa 12 na Mtwara 1 nao wataambatana na vijana wengine toka Makanisa mbalimbali ya Waadventista Wasabato kwa Divisheni ya Mashariki mwa Afrika na Mgeni Rasmi akiwa ni Mchungaji Baraka Muganda toka chuo cha Waadventista Wasabato Washington Malekani..

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA