Tafakari Ya Leo - 2Nyakati 20:14-15
Ndipo Yahazaeli mwana wa Zekaria .... Akajiliwa na Roho ya Bwana katikati ya kusanyiko; akasema , sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; BWANA awaambia hivi, MSIOGOPE, wala MSIFADHAIKE kwa ajili ya Jeshi kubwa hili; kwani vita si YENU bali ni ya MUNGU.
TAFAKARI: NI WAKATI WA KUSHINDA VITA NI BWANA
Mpendwa! leo nina habari njema kwako, ya kwamba Mungu anajua pambano ulilonalo katika Maisha yako, tangia mwanzo, mwanadamu wa kwanza alipoasi, wanadamu wote wanapitia changamoto fulani katika maisha. Pamoja na baadhi ya watu kuishi maisha mazuri yakiwa na mafanikio tele, bado katika safari ya maisha kuna pambano la aina fulani. Kama si la Kiroho basi la kimwili.
Mtu fulani anaweza kudai hana Pambano, lakini kuishi maisha ya dhambi huku akijiita Mtu wa Dini hilo ni pambano, kwa sababu nia yake ni kuokolewa lakini Adui shetani amemshinda amekuwa mateka akitelemkia kuzimu. Wewe unayeugua bila kupona hilo ni pambano, wewe unayesumbuka na Ndoa yako, badala ya kuishi kwa Raha unaambulia karaha au kutengana, hilo ni pambano. Wewe unayeteseka kwa kukosa mchumba au kudanganywa na matapeli wa mapenzi, hilo ni pambano. Wewe unayetafuta kazi hupati, biashara mtaji huna au zinaporomoka kila kunapokucha, hilo ni pambano.
Wewe uliyekosa ada ya chuo au umekosa credit za kuingia chuo, na wewe uliyeko chuoni lakini walimu wanakulamizimisha utoe rushwa ya Ngono ili ufaulu mitihani, hilo nalo ni pambano. Wewe unayeonewa kazini, hupandishwi cheo na kupewa mshahara usioendana na Kazi, hilo ni pambano. Wewe unayeonewa na Mashetani, usiku hulali unasumbuliwa na wachawi, umetupiwa majini ya mikosi, unasumbuliwa na majini mahaba usiku, magonjwa ukipima hospitali hawaoni, mikosi na laana vinakuandama, hata familia na jamii wanakutenga, hayo yote ni Mapambano.
Vijana wa kiume waofaidi maisha kwa kufugwa na Majimama (Sugar Mameee) na Vijana wa Kike wanaoishi kwa kutoa huduma za Nyumba ndogo na kujisifia kuwa ATM zao (Mabuzi) hayaishiwi Pesa, yote hayo ni mapambano tu. Wale wote wanaotumia Madawa ya kulevya, bangi na kila aina ya Vileo, yote hayo ni Mapambano – kwa sababu hata wakitaka kuacha au wakitamani kujitoa na maisha hayo wanashindwa.
Inawezekana sijataja pambano ulilonalo, isikupe shida, sikiliza sauti ya Mungu ikisema: Pambano au Vita hiyo si Yako bali ni ya Mungu, Haya simameni kwa Ujasiri mwambieni Bwana timiza neno lako kwangu. Shetani alishashindwa, hana uwezo wala mamlaka kwa watu wa Mungu, fanya uamuzi mruhusu MUNGU atawale maisha yako - UTAIMALIZA SAFARI YA MAISHA YAKO KWA USHINDI MKUBWA.
NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO, NA UPENDO WA MUNGU BABA NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU -UKAE NASI SOTE SASA NA HATA MILELE.
By Ev. Eliezer Mwangosi

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment