Wanafunzi sabini na watatu (73) wameweka rekodi ya
wanafunzi wa kisabato kubatizwa katika shule moja mwaka huu katika kisiwa cha
vanatu. Idara ya vijana katika kisiwa cha vanatu imeripoti kua lilifanyika juma la Maombi shuleni lhapo kwa muda
wa wiki tatu katika shule hiyo na liliongozwa na mchungaji Charlie Jimmy pia
wanafunzi hao waliweza kuyapenda masomo
hayo nakuanza mafunzo ya kujifunza biblia rasmi kwa ajili ya ubatizo
Pia kutokana nawanafunzi
kukubali masomo hayo mwezi oktoba mwaka huu mchungaji Charlie Jimmy
ambaye anafanya kazi katika ofisi ya mkuu Mission ya Vanuatu katika Port Vila,
walirudi kisiwa cha Santo kubatiza wanafunzi ambao walimkiri Yesu
kua Bwana na Mkombozi wa Maisha yao.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo ya Aore Alisema “Amefurahishwa sana kuona kua wanafunzi hao
wame mpokea Yesu na kumkiri kua ni Bwana na Mkombozi wa Maisha yao “Pia
aliongezea nakusema kua wanafunzi hao wamekua mfno mkubwa katika shule hiyo na
si katika masomo darasani hata katika
upande wa kiroho.





0 comments:
Post a Comment