Sunday, December 07, 2014

WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam.
Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.
Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto(kulia)  na kushoto ni mwenyekiti wa Family Singers Mr.Jonas wakiongea na waandishi wa Habari. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Mwenyekiti wa Family Singers nae akisema neno katika mkutano na waandishi wa habari..
Aliwataja waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC (T) Vijana Chang’ombe, Acacia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.
Misheto ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693**

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA