MISSION EXTRAVAGANZA
Huu ni mkutano mkubwa unaowaleta pamoja viongozi wa ngazi za juu za kanisa na viongozi wote wakuu wa divisheni ya Afrika Mashariki na Kati kwenye sherehe kuu ya matukio mbalimbali ya kiuinjilisti. Mkutano huu unafanyika katika jiji la Dar es Salaam ambapo unakadiriwa kuhudhuriwa na viongozi 500,000. Mkutano huo utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa unakadiriwa kuhudhuriwa na watazamaji 50,000. Moja ya mambo makuu yaliyo kwenye ratiba ni ubatizo mkuu wa pamoja utakaofanyika Bahari ya Hindi kati ya tarehe 4 na 7 ya mwezi wa Februari 2015, utakaojumuisha wabatizwa wa hapa nchini na wa eneo zima la Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati.
MAANDALIZI YA EXTRAVAGANZA
Ili kupata wabatizwa wa hapa kwetu, imependekezwa kuwa na Mikutano ya Injili katika eneo la Jiji la Dar es Salaam na sehemu ya mkoa wa Pwani kuanzia 10 hadi 31/2/2015 (kipindi cha majuma matatu) kwa utaratibu kama ule uliotumika kwenye mikutano iliyofanyika mwezi wa sita kukiwa na uboreshaji wa yale maeneo yaliyokuwa na upungufu. Mkutano huu utakuwa wa Union Misheni ya Kusini mwa Tanzania ikishirikiana na Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania. Mikutano kama hiyo hiyo pia inahimizwa kufanyika katika maeneo mengine ambayo Konferensi husika itayachagua katika tarehe itaazoona zinafaa.
Katika mikutano hii ya Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake, kila kanisa na kila kundi litakuwa kituo cha mkutano. Tunatarajia kuwa na vituo visivyopungua 145. Kanisa mahalia litapendekeza wahubiri watakaosimama katika vituo vyao kutoka kokote ndani ya kanisa letu na kuyatuma mapendekezo hayo ofisi za ETC, mapema kwa ajili ya kuwaombea kibali wale walio nje ya Konferensi. Tunatarajia nusu ya wahubiri wawe wachungaji na nusu nyingine ya walei. Vituo vitakavyopewa wahudumu na Union ama Konferensi vitasaidiwa kuwasafirisha wahudumu hao bali huduma za chakula na malazi zitakuwa juu ya kituo.
Kamati mbalimbali za kufanikisha mkutano huu ziundwe na kuanza kazi kuanzia sasa, nazo zitaendelea na shughuli zake hadi mkutano utakapokwisha. Ili kuleta ufanisi mkutano utafanyika kwa majuma matatu na matayarisho kwa majuma matatu mfumo tuliouita 1, 2, 3. Juma la kwanza litakuwa la uamsho wa washiriki kwenye kanisa au kundi mahalia, wenye lengo la kuwaonyesha umuhimu wa kazi ya injili na namna ya kuifanya kazi hiyo. Uamsho huo utaanza tarehe 20 Disemba 2014 nao utaendelea hadi tarehe 27 Disemba 2014 ukifanyika asubuhi na jioni ukiendeshwa na mtu maalumu aliyeteuliwa na kanisa. Mwisho wa juma hili wito utatolewa wa wale walio tayari kutafuta na kuleta roho moja katika mkutano huo. Watu hao wataandaliwa fomu maalumu ambayo wataisaini. Sambamba na hao wito mwingine utatolewa wa wale walio tayari kuwalea waongofu watakaopatikana ambao nao watapewa fomu maalumu watakazozisaini. Majina ya makundi yote mawili yatajadiliwa na baraza la kanisa na kupitishwa.
Majuma mawili yanayofuata yaani kuanzia tarehe 27 Disemba 2014 hadi tarehe 10 Januari 2015, kutakuwa kuingia nyumba kwa nyumba kwa lengo la kufungua na kuendesha madarasa ya Biblia Yasema na Sauti ya Unabii. Kila kituo kitapewa seti 20 za masomo ya Sauti ya Unabii na vitabu 10 vya Biblia Yasema kwa ajili ya kufundishia madarasa yatakayofunguliwa. Mahubiri yataandamana na matukio mbalimbali ya kuihudumia jamii kama kusafisha mazingira, kukarabati maeneo korofi ya barabara muhimu, kutembelea vituo vya kulelea yatima na wenye mahitaji maalumu, kutembelea hospitali na magereza, kufanya sabato za wageni, kuwaalika wenye mahitaji maalumu kanisani, kugawa tumaini kuu na Sabato ya Kweli, kugawa vijizuu, kutoa elimu ya ndoa na familia, kutoa elimu ya Computer, kutoa elimu ya afya, huduma za upimaji, na matibabu.
Mikutano ya hadhara itahitimishwa tarehe 31/01/2015 na kufuatiwa na ubatizo wa pamoja utakaofanyika Bahari ya Hindi, wakati waliohitimu masomo ya Sauti ya Unabii watafanyiwa mahafali yao maalumu, Uwanja wa Taifa wakati wa Tamasha la Utume.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment