Friday, January 30, 2015

Simulizi hizi muhimu zitakuwa zinakujia kwa siku 3 yaani Jumatano,ijumaa na jumapili.                             
        Imeandaliwa na Mch J.Kuyenga
                Historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato katika sehemu za     kati,Mashariki,Kusini na magharibi mwa Tanzania.
Jaribio la kuuzima moto wa injili ya Kiadventista Mjini Morogoro
Mwaka 1960 Union ilituma timu ya wahubiri chini ya uongozi wa Pr.Fares M.Muganda kuendesha mahubiri makubwa hapa Morogoro.
Baada ya maandalizi walitangaza kufungua mahubiri yao katika jengo la Shan Sinema.Matangazo haya yaliwaleta watu wengi sana katika jengo hilo la Sinema,Pr.Muganda na timu yake wakaanza mkutano kwa kujitambulisha na kwamba walikuwa wamepewa kibali kuendesha mikutano hiyo.Ghafla maswali yakaulizwa.Majibu yalipotolewa yaliamsha kelele katika mkutano na vurugu na kutishia kuwaua wahubiri hao,vurugu zikawa kubwa kiasi cha kuvunja viti na ndipo kila mtu alitawanyika kwa njia aliyoipata mwenyewe na wahubiri wakatoroka.Na mwenye ukumbi akatangaza kwamba mikutano hiyo haitaendeshwa katika ukumbi wake.Hata hivyo wahubiri hao waliendesha mahubiri kimya kimya katika majengo ya Labour Office,lakini hayakuwa na matokeo mazuri,kisha timu yote ilitawanyika na kumwacha Pr.E.Wanjara peke yake hapa mjini.
Akashirikiana na mwinjilisti Lukwaro,waliendelea kuhubiri nyumba kwa nyumba na kujipatia baadhi ya washiriki waliokuwa wakiishi hapo,kwa mfano Nyambabi,Daniel Mwakyusa  na Godfrey Suleman wakaanza kusali katika jengo la welfare.
Pr.Wanjara alitumia muda mwingi akihubiri huko Mpwapwa na kuanzisha kanisa huko,akishirikiana na Mwinjilisti John Lyambwa.Washiriki kama Yohana Chilungwana,Wilson Mogoire n.k ni matokeo ya kazi yao.
INAENDELEA JUMAPILI 
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA