Friday, January 02, 2015

 Na mwandishi wetu
Ibada iliyofanyika katika kanisa la Magomeni SDA kuukaribisha mwaka mpya wa 2015,ilikuwa na mbaraka wa aina yake kwani familia ya Mr na Mrs Mafuru walibatizwa kwa maji katika kisima cha ubatizo kilichopo kanisani hapo.
Tafakari ya maandiko matakatifu iko wazi juu ya neno"KUZALIWA MARA YA PILI" hili huonekana pia katika kipindi cha Yesu ambapo mfarisayo mmoja enzi za Mwokozi,aliyeitwa Nikodemo alitamani sana kufahamu ni namna gani mtu azaliwe tena kwa mara pili.
YOHANA 3:3-5
 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Mzee wa kanisa la Magomeni Ezekiel Mkundi akiwaapisha wanafamilia hao(hawako pichani) kwa kuwauliza maswali.
Mzee wa kanisa la Magomeni Ezekiel Mkundi akiwaapisha wanafamilia hao(hawako pichani) kwa kuwauliza maswali.
Wanafamilia Mr na Mrs Mafuru wakiapishwa na kupokea kiapo hicho siku ya kuupokea mwaka mpya 2015 ndani ya kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni
Mchungaji wa mtaa wa Magomeni sda,Jonas Singo akiingia ndani ya kisima cha ubatizo tayari kwa huduma hiyo..
Wanafamilia wakisali pamoja na Mchungaji kabla kabla ya huduma ya ubatizo.
Mchungaji Jonas Singo hapa alitoa ombi tayari kwa huduma ya ubatizo
Huduma ya ubatizo ndio ilifanyika hivi naye Mrs Mafuru akipokea ushirika wake kwa njia ya ubatizo katika kisima cha ubatizo kanisani Magomeni sda..
Mchungaji Singo alipata kuomba katika kuanza kwa huduma ya ubatizo,akiwa na Mrs Mafuru
.Mafuru azaliwa upya kwa kubatizwa katika kuzamishwa maji mengi.
Wanafamilia wakitoka nje ya kisima mara baada ya huduma ya ubatizo wa aina yake kwa kuanza mwaka 2015.












****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0789 243 413 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA