Friday, January 23, 2015

MKATABA wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM) ulitiwa saini usiku wa jana, Jumatano, Januari 21, 2015, katika sherehe ya kufana iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ngurdoto, .
Sherehe hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kimesimamia mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo. Rais Kikwete pia ndiye mdhamini mkuu wa Mkataba huo.
Mkataba huo pia unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinabuni na kutekeleza sera za kuondokana na ukabila, makundi yenye mitazamo finyu na mwenendo wa kijeshi katika siasa za Sudan Kusini.
Aidha, Mkataba huo unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinafanya mageuzi ya kuanza kujenga utamaduni wa kuvumiliana na ujenzi wa misingi ya demokrasia.
Mkataba huo pia unataka watu wote ambao walishiriki katika mauaji na umwagaji damu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wasiruhusiwe kugombea wala kushika nafasi ya uongozi wa umma ndani ya chama hicho.
Pia viongozi wote wa Sudan Kusini wanatakiwa, chini ya Mkataba huo, kuwaomba radhi wananchi wa nchi hiyo ya Sudan Kusini kwa kuruhusu nchi hiyo kuingia katika machafuko ya umwagaji damu mkubwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
22 Januari,2015

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akikaribisha viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo akisoma muhtasari wa mazungumzo hayo


 Sehemu ya ukumbi wa mkutano huo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini wa  Mhe. Salva Kiir Mayardit  Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD). 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol

baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na

kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na

kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

 Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiongea
 Dkt. Riek Machar akiongea 
 Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiongea
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Bw. Bw. Deng Alor Kuol  wakifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
 Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini
 Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Kikwete na Bw. Dkt Kuol wakipiga makofi wakati  Rais Salva Kiir Mayardit  wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha

upya chama cha SPLM cha Sudani Kusin

 Naibu Rais wa Afrika ya Kusini Mhe Cyril Ramaphosa akiongea na kupongeza hatua iliyofikiwa
 Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Wajumbe wa kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)


 Sehemu ya wajumbe wa kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
 Kila mtu alisimama kumshangilia Rais Kikwete
 Wajumbe wa  kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD)
 Furaha kwa kila mtu
 Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo akisoma dondoo za makubaliano
 Meza kuu katika picha ya pamoja na kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG)
Picha ya pamoja na kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
 Picha na Sekretareti ya mazungumzo hayo
 Rais Kikwete na Mzee Malecela wakipongezana baada ya kufanikisha mazungumzo na hatimaye makubaliano ya viongozi wa SPLM
 Rais Kikwete akishukuru vikundi vya ngoma za utamaduni vilivyokuwapo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kumsindikiza  baada ya mkutano wa mafanikio
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA