Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Dr Ted Wilson
amewasili Juba,Sudan ya Kusini akitokea nchini Tanzania baada ya
kushiriki kwenye sherehe za utume wa kanisa hilo(Mission Extravaganza)
zilizofanyika kwa juma zima toka februari mosi mwaka huu na kuhitimishwa
kwenye uwanja wa Taifa kuanzia Februari 4 hadi 7,mwaka huu. Ted akiwa
nchini Tanzania aliongoza ibada ya siku ya Sabato ambapo alihutubia
waumini wa kanisa hilo wapatao 50,000 wanaounda Divisheni ya Afrika
Mashariki na Kati yenye nchi 11,huku ukihudhuriwa na Makamu wa Rais Dr
Mohamed Gharib Bilal ambaye alizindua mkutano huo akiwataka waumini hao
kuombea taifa la Tanzania kudumisha amani,upendo na mshikamano. Mkutano
huo ambao pia ulihudhuriwa na viongozi wandamizi wa Kanisa la
Waadventista Wa Sabato toka yalipo makao makuu yake huko Washngton
DC,Marekani ulishuhudia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Bernad Membe akiufunga kwa kulipongeza na kulitaka kanisa
hilo kutojiingiza katika migogoro ya aina yoyote. Ted Wilson akiwa
ameambatana na viongozi wengine wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati
aliwasili Juba na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo
nchini humo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kutembelea nchini
hiyo toka ilipojitenga na Sudani julai 9,2011.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***









0 comments:
Post a Comment