Akiweka wakfu jengo la kanisa la Ilala sda hapo jana Mchungaji Ruguri amesifu juhudi za washiriki wa kanisa hilo kwa kupendezesha kanisa na kuweka vito vya thamani ndani ya kanisa hilo,pia asema ni kimbilio la wasumbukao,ni mahala ambapo utetezi wa dini hufanyika na kanisani pia ndio usuluhisho kwa matatizo kadhaa ndani na nje ya kanisa hufanyika.
MUHTASARI WA SHUGHURI ZA UJENZI WA KANISA1993-KUWEKWA JIWE LA MSINGI WA KANISA MCHUNGAJI JOKTANI KUYENGA
2005-KUWEKA TARAZO
2009/2010-KUJENGA MIMBARI
2010/2011-KUWEKA UMEME NA KUFUNGA BANDERING KWA AJILI YA GYPSUM
2012-KUEZUA MABATI YA ZAMANI,KUEZEKA BATI LA MGONGO MPANA,KUFUNGA GYPSUM,KUWEKA VIOO VYA VERANDA.
2014-KUWEKA VIOO VYA MADIRISHA,KUFUNGA TILES NDANI NA KUPAKA RANGI NJE
 |
Mchungaji Ruguri akiwa na Mke wake katika tukio la uwekaji wakfu jengo la kanisa la Ilala hapo jana mchana. |
 |
Mchungaji Ruguri akitambulisha hati ya kanisa la Ilala kabla ya kuikabidhi kwa uongozi wa kanisa hapo jana. |
 |
Mke wa Mchungaji mama Elizabeth akitoa hati ya kanisa kwa Mchungaji na wazee wa kanisa la Ilala mapema jana katika sherehe za uwekwaji wakfu. |
 |
Mchungaji Ruguri aakiwa na mke wake pamoja na viongozi toka division,union na konferensi wakielekea katika jiwe la uwekwaji wakfu kanisa la Ilala sda. |
 |
Kushoto mama Elizaberh Ruguri mke wa Mchungaji Ruguri na kulia ni Mchungaji Blasious Ruguri wakiwa na shauku ya kufanya jambo kubwa la kuweka wakfu kanisa la Ilala sda. |
 |
Kushoto ni Mchungaji Blasious Ruguri akisema jambo mara baada ya kuweka wakfu jengo la kanisa la Ilala na kulia ni mke wake mama Elizaberh Ruguri. |
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment