Mwanasheria Mkuu wa Marekani Eric Holder |
Mwanasheria Mkuu wa Marekani Eric Holder amesema
kuwa uchunguzi mkubwa uliofanywa kuhusu mauaji yaliyofanywa na polisi
mzungu dhidi ya kijana mweusi ambaye hakuwa na silaha katika mji wa
Ferguson kwenye jimbo la Missouri umebaini kuwapo mfumo wa kibaguzi
dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika (weusi).
Holder aliyasema hayo jana baada ya Wizara ya Sheria kumfutia tuhuma za mauaji afisa wa polisi Darren Wilson aliyemfyatulia risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown.
Holder aliyasema hayo jana baada ya Wizara ya Sheria kumfutia tuhuma za mauaji afisa wa polisi Darren Wilson aliyemfyatulia risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani ameituhumu Idara ya Polisi ya Ferguson kuwa imetengeneza mazingira yenye sumu kali katika mji huo wa jimbo la Missouri ambako Brown alipigwa risasi na kuuawa bila ya hatia yoyote Agosti 9 mwaka jana.
Vilevile Wizara ya Sheria ya Marekani imetoa ripoti kuhusu jinsi polisi ya mji wa Ferguson ilivyojenga hofu na chuki kati ya Wamarekani weusi wa Missouri kwa kuwawekea faini na kutumia mabavu na nguvu zaidi.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani amesisitiza kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi unashuhudiwa kwa kiwango kikubwa na cha juu.
0 comments:
Post a Comment