Friday, March 06, 2015


Rais Kikwete akizungumza na wawakilishi kutoka Chama cha Albino Tanzania
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amekutana na Viongozi wa Chama cha Watu wenye Albino Tanzania na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuongeza nguvu ili kumaliza tatizo la amauaji ya dhidi ya Albino."Mauaji haya yanaisikitisha Serikali na kuifedhehesha sana, msidhani hatufanyi lolote, tunafanya juhudi kubwa na mbalimbali lakini imefikia wakati tuongeze juhudi hizo"alisema Rais.
 Katika kikao hicho viongozi wa watu wenye Albino nchini wamesoma risala ambayo imetoa kilio chao na mapendekezo yao kwa serikali na hatimaye ikaafikiwa kuwa na haja ya kuunda kamati ya pamoja ambayo itajumuisha Serikali, viongozi wa watu wenye Albino, viongozi wa waganga wa jadi na wadau wote wakuu katika suala hili ili kupata mapendekezo na mkakati wa pamoja ambao hatimaye mauaji haya kukomeshwa kabisa nchini Tanzania.

katika kikao cha Jana, viongozi wametoa kilio chao kwa serikali kuziangalia na kuzimulika taasisi zisizo za kiserikali ambazo pamoja na kujipambanua kuwa zinatetea haki za watu wenye Albino nchini bado hazina mkakati wa pamoja na hazipo wazi kwa walengwa hapa nchini.Mapema jana asubuhi mara baada ya kufika Ikulu, kulitokea sintofahamu baina ya viongozi wa Chama cha Watu Wenye Albino na watu wasio wanachama kwa kile kilichoelezwa kuwa uongozi huo sio halali kwa vile muda wake umeshakwisha wa kukaa madarakani.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Albino, Ernest Kimaya ameelezea masikitiko kwake kwa Rais na kuelezea kuwa uchaguzi haukuweza kufanyika kutokana na ukosefu wa fedha na wamemuomba Rais awasaidie kutimiza azma yao ya kuitisha mkutano na kuchagua viongozi wa Chama chao.ulingana na Bw. Kimaya wamepanga kufanya mkutano huo wa kuchagua viongozi katikati ya mwaka huu ambapo pia dunia itakua inaazimisha siku ya watu wenye Albino duniani.

Rais amekubali ombi hilo na hiyo itazungumzwa kwa urefu katika kamati ya pamoja ambayo inatarajiwa kuwa imekamilika wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA