Gari la Dr. Slaa likiwa limepaki nje ya Kituo cha Polisi Central. |
Waandishi wa habari (kulia) wakimsubiri Slaa nje. |
..Slaa(kulia), akitoka katika lango kuu la kituo cha Polisi akiwa na viongozi wengine wa chama hicho. |
Akihojiwa
na Wanahabari.KATIBU Mkuu wa Chadema, Dr. Willbroad Slaa, ameripoti
katika Kituo cha Polisi Central kilichopo Posta jijini Dar kuhusiana na
sakata zima la mlinzi wake anayetuhumiwa kutaka kumuua.
Akizungumza
na wanahabari kituoni hapo, Slaa alisema yeye hakuitwa na Jeshi la
Polisi kujielezea bali kutokana na maneno yanavyozidi kusambaa na
kuwasilishwa ndivyo sivyo ameona aende kueleza ukweli ulivyo.
Alisema
kuwa, kwa mujibu wa chama chake, ameona ni vyema kwenda kulieleza Jeshi
la Polisi kuhusiana na ishu nzima inayomkabili mlinzi wake, ambapo
alikutana na Kamanda wa Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Suleimani
Kova na kumueleza kila kitu kwa kuandika karatasi tisa (9) zenye maelezo
yake, hivyo zoezi zima la kutoa taarifa kuhusiana na alichoandika
ameliachia Jeshi la Polisi baada ya wao kufanya kazi yao ya Uchunguzi.
“Ndugu
zangu wanahabari sijaitwa hapa kwa ajili ya mahojiano kama taarifa
zinavyozaga lakini kutokana na uongozi nilionao nimeona ni vyema suala
hili nilifikishe Polisi, na katika maelezo yangu nimeweza kuandika zaidi
ya karatasi tisa (9) zenye ukweli mtupu, hivyo nimelikabidhi Jeshi la
Polisi na baada ya wao kufanya uchunguzi litatoa taarifa kamili juu ya
kile nilicho kiandika,’’ alisema Dr. Slaa.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment