Uchunguzi wa chembechembe za DNA umehakikisha kuwa ni mwili wa shahidi wa mahakama ya ICC |
Bwana Yebei alitarajiwa kuwa shahidi wa mshtakiwa
kwenye kesi dhidi ya Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, anayekabiliwa na
mashtaka ya mauaji katika mahakama hiyo ya kimataifa huko Hague.Gazeti
moja la Kenya limemnukuu afisa wa uchunguzi akisema kwamba chembechembe za DNA
zimedhibitisha kwamba mwili huo uliopatikana ni wa Yebei.
ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi
na makazi salama lakini akakataa Matokeo haya ni sambamba na yale
yaliyochapishwa na daktari mmoja wa Afrika Kusini aliyepewa kazi hiyo na
familia.Inatarajiwa kuwa serikali sasa itafanya uchunguzi wa pili kugundua
kilichosababisha kifo chake.
Inasemekana kwamba Meshack Yebei alitekwa nyara mwishoni mwa
mwezi Desemba nyumbani kwake Eldoret alipokwenda kumwona mkewe ambaye alikuwa
anaugua.ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na
makazi salama lakini akakataa.Mwezi Januari mwili ulioharibika vibaya
ulipatikana katika mto ulio takriban kilomita arobaini kutoka nyumbani kwake,
na familia ikadhani kuwa ni yeye.
ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa |
Mbuga ya Wanyama ya Tsavo, ambako mwili huo
ulipatikana, iko takriban kilomota mia sita kusini mashariki mwa Eldoret
alikotoweka.Aidha familia yake imelalamika kuhusu muda ambao serikali imechukua
kutangaza matokeo ya DNA, na imetishia kuuchukua mwili huo ili iuzike wiki hii,
iwapo serikali itatoa thibitisho hilo au la.
0 comments:
Post a Comment