Ripoti ya mashirika zaidi ya ishirini ya misaada ya kibinadamu na yale ya kutetea haki za binaadamu yamelishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kutetea raia walio katikati ya vita nchini Syria.
Ripoti hiyo imezishutumu nchi zenye nguvu kubwa ya ushawishi duniani kwa kushindwa kutumia nguvu zao kuandaa maazimio ya kusaidia uhuru wa huduma za misaada ya kibinadamu kwa waathirika.Ripoti ya masharika hayo ni ya kuadhimisha miaka minne ya vita nchini Syria ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa.David Milband ambaye ni Rais wa Shirika la kimataifa la Uokoaji International Rescue Committee amesema kuna ongezeko dogo la misaada inayotolewa kuwasaidia raia wa Syria.
0 comments:
Post a Comment