Sunday, April 26, 2015

Ikiwa ni kumbukumbu ya kile kilichofanyika miaka zaidi ya 50 iliyopita, leo katika jiji la Dar es Salaam Sherehe za muungano zikiongozwa na raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wengi waliodhuria pamoja na wananchi zimefana. Pata angalau kilichojili kwa kutazama picha hizi..
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo.
 Picha na OMR

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA