Tuesday, April 28, 2015

Akiongea mbele ya mamia ya waumini waliohudhuria ibada takatifu ya sabato kutoka katika viunga vya jiji la Mwanza iliyohudhuriwa pia na watoto waishio katika mazingira magumu wanaolelewa na shirika lisilo la Kiserikali la Foundation Karibu Tanzania, ujumbe mahususi ulikuwa :-MFUNZE MTOTO LEO JENGA KANISA LA KESHO
Mathayo 18:1-6; mark 9:35,36,37;luka 10:25,26 yohana 15:3-17
Watoto ni vito vya thamani ambavyo mara nyingi tumekuwa hatuwatendei inavyostahili kama ambavyo wanafunzi wa Yesu walitaka kuwafukuza ,Marko 10:13-16, lakini Bwana Yesu kwa kutambua ya kwamba watoto ni vito vya thamani aliwaambia wanafunzi wake kwamba,walio mfano wa hao wadogo ufalme wa Mbinguni ni wao. Yesu anapenda tudumishe uhusiano na watoto na hatimaye wamwelekee Mungu huku wakikua katika hekima na kimo. Bwana anachukizwa na namna ambavyo hatuwajali watoto .
Nani aliye mkuu katika ufalme wa Mungu? Mathayo 18:1-6
Watoto walioandaliwa vizuri wakiunganishwa na Yesu hufanya mambo makubwa na Bwana anakuwa mbaraka kwao. Kama wazazi twapaswa kuwalea watoto katika njia inayopasa hata watakapokuwa watu wazima na hatimae wawe warithi wa ufalme wa Mbinguni. Upendo, Usalama,malezi na makuzi ya watoto ni jukumu letu wazazi.
Tukikaa ndani ya Kristo na Kristo ndani yetu, tutakuwa na upendo ambao utatupatia hekima ya kuwalea watoto wetu na hatimaye kumpendeza Mungu na wanadamu pia.
Sabato hii ya ukarimu ya watoto iliyoandaliwa na kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba pia tumeshuhudia watoto waishio katika mazingira magumu wanaolelewa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation Karibu Tanzania wakishiriki chakula pamoja na watoto wenzao kanisani,zawadi mbalimbali zilitolewa kama nguo za watoto wachanga(nepi),vifaa vya michezo,madaftari ,juice,mabegi ya shule,kalamu, mashine ya kunyolea nywele,dawa ya kusafishia maliwatoni, kontena za kuhifadhi chakula,tolori kwa ajili ya kusombea taka ,fedha tasilim na vitabu vya neno la Mungu.
Mchungaji Heri Mramba wa mtaa wa Kirumba, alihitimisha siku hii makini kwa kutoa huduma ya kubariki watoto ambao pia walisindikizwa na
wazazi\walezi wao.
Habari/picha na Kirumba sda Facebook Page










****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA