Watoa huduma za uokoaji huko mji
mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri
wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya funikwa na vifusi vya jengo
alilokuwemo wakati wa tetemeko la ardhi kukumba taifa hilo siku tano
zilizopita.
Licha ya kuwa chini ya maporomoko hayo kwa siku hizo
tano isaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua
japo kwa shida.Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake.Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.
Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo.
Wengi wa wanavijiji wangali wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa huku mashirika ya kutoa misaada ya kisema huenda ikachukua siku nyengine 5 kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa miundo mbinu.
Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415 kuisaidia Nepal katika kipindi cha miezi 3 ijayo. Chanzo na BBC
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment