Friday, May 01, 2015


Ban Ki-moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea tahadhari yake kuhusiana na hatari ya raia kuendelea kupigana, Nchini Yemen.
Anasema kuwa zaidi ya watu elfu moja mia tano wameuwawa na wengine laki tatu wametoroka makazi yao, katika kipindi cha majuma sita yaliyopita.
Mashambulizi katika majumba ya raia zikiwemo hosptali na maghala ya vifaa vya misaa ya kibinadamu yamekuwa yakiendelea.
Mapigano huko Yemen
Kumekuwa na taarifa watu wenye silaha wamekuwa wakiwateka raia katika mitaa ya Aden.
Shirika la Umoja wa mataifa la misaada ya chakula limesema halina jinsi zaidi ya kusitisha mipango yake ya kusambaza misaada kutoka na tatizo la mafuta.
Kwa sasa mapigano makali yanaendelea katika mipaka ya eneo la Yemen na Saudia Arabia. Taarifa na BBC

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA