Sunday, May 31, 2015

Kaimu Mkurugenzi wa Idaraya Afya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania (NTUC), Dk Silas Kabhele, amesema zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu zimetumika kujenga Hospitali hiyo.
Aidha,Dk.Kabhele amewomba wadau wote wa Huduma za Jamii kuchangia mradi huu toka kona zote za nchi kuingiza michango yao katika akaunti ya ujenzi wa hospitali hii:
Jina la akaunti: Pasiansi SDA Hospital Fund,
Akauntinamba:      01J1060067500
Benki: CRDB
Picha ya Jengo la Hosptali ya Pasiansi inavyoonekana mara itakavyokamilika
 Dk.Kabhele ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya katika Jimbo  la Kusinim wa Ziwa Nyanza(SNC) amesema Siku ya Sabato Mei 30 kwamba sasa zinahitajika takriban shilingi milioni 600 kukamilisha ujenzi.
Akizungumza wakati wa Huduma Kuu katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba Jijini Mwanza,Dk.Kabhele amesema Hospitali hiyo ya Gorofa tano tayari paa limeezekwa,kuta zote za nje zimepigwa lipu; na kwamba hata baadhi ya kuta za ndani zimepigwa lipu.
“Takriban shilingi bilioni 1.6 zimekusanywa kutoka kwetu na kutoka kwa rafiki zetu; kazi zilizobaki ni kumalizia lipu ndani, kuweka sakafu, madirisha, milango, kupakarangi, kuingiza umeme na maji na kusimika mitambo ya usalama”,Dk. Kabhele amebainisha.
 Aidha, amesisitiza kuwa Hospitali itakapoanza kazi, itakuwa kituo cha  Uinjilisti, ambayo ndiyo njia ya pekee ya kuisaidia jamii isiyomjua Mungu kuja wenyewe kwaYesu Kristo.
“Wale ,hujakutafuta huduma ya Afya; na hivyo hupata Injili itakayokuwa ikitolewa sambamba na huduma zetu za afya”,Dk. Kabhele amesisitiza. 
Jiwe la Msingi la Hospitali hiyo liliwekwa na Rais Jakaya Kikwete Septemba 8 mwaka 2013; na Hospitali hiyo ilitazamiwa kufunguliwa rasmi mwaka huu wakati wowote ikikamilika.
Akizungumzia vifaavya tiba,Mkurugenzi huyo wa Afyaamesema, tayari Kontena mbili za vifaa vimekwisha tumwa kutoka Uswisi, na Wajerumani wameahidi kuleta vingine kwa ajili ya kuanza kazi baada ya ujenzi kukamilika.

Kulingana na Kamati ya Ujenzi, kila Mtaa katika Jimbo la SNC umepangiwa goli lake.
 Hospitali hiyo itakapokamilika, itakuwa na vyuo mbalimbali vya Sayansi ya Tiba, na itakuwa na uwezo wa kuhudumia wastani wa wagonjwa 200 kila siku, pia itakuwa na jumla ya vitanda 450  vya kulaza wagonjwa.

Habari/picha na KIRUMBA SDA BLOG
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA