Sunday, May 17, 2015

Juma la Elimu lafana Kirumba
• Taasisiza Waadventista zabainishwa kuwa vituo vya Uinjilisti
Na ShuhudaWetu,Kirumba
JUMA LA ELIMU limefika kilele chake Sabato ya Mei 16 mwaka huu 2015 katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba Jijini Mwanza, likihimiza Jamii ya Kitanzania kutambua kuwaTaasisi za Elimu zinazomilikiwa na Kanisa hilo nivituo vya kufundisha na kuhimiza maadili bora kwa Jamii.
Tangu Mei 9 hadi 16 mwakahuu,Juma hilo lilikuwa likiendelea Kanisani Kirumba,likiwahimizaWaumini wa Kanisa la Waadventistawa Sabato hapa nchini kuthamini Elimu na Taasisi za Kanisa,ambazo zimejidhihirisha kutoa Elimu na malezi bora hapa Tanzania.
Akihubiri wakati wa Ibada Siku ya Sabato, Mwalimu wa Taaluma Shule ya Sekondari Nyanza,inayomilikiwa na Jimbo la Nyanza Kusini(SNC) la Kanisa la Waadventista wa Sabato,Isaac Mwailafu, amesema Waadventista wa Sabato sasa wanatakiwa kutumia vema fursa zinazopatikana.
Mwalimu Mwailafu amesema muda uliobaki wa kuhubiri HABARI NJEMA nimfupi,waumini wa Kanisa letu wanapaswa kutumiaTaasisi za Elimu za Kanisa kama VITUO VYA UMISIONARI.
Kulingana na Utafiti uliofanywa hivi karibuni,Shule na Vyuo vya Waadventista,ndiko mahali sahihi jamii inakopata elimu na malezi ya kuwawezesha kulitumikiaTaifa kwa uaminifu na uzalendo katika zama hizi za mmomonyoko wa maadili na ufisadi.
“Vituo hivi tunaweza tukavipuuza.
Lakini, Bwana ameviinua”Alisema hukuakisisitiza,
“Mfano, Chuo Kikuu cha Andrews kilichoko Marekani kilianza mwaka 1874;kinaumriwamiaka 141;wakati kilianza kikiwa banda la mbao,wakati sasa Chuo Kikuu hiki ni kati ya vyuo vikuu 10 bora Marekani”,amesema mwalimu huyo.
Akasema, leo Chuo Kikuu hicho kina miliki eneo kubwa;najina lake linatokana na Mchungaji aliyeweza kukariri Agano Jipya kichwani mwake.Chuo hiki hupokea wanafunzi zaidi ya 3,500 duniani kote.
Kufuatia hali hiyo,Mwalimu Mwailafua kawataka waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato kuheshimu na kuthamini shule zinazomilikiwa na Kanisa.
Shule yaNyanza,lichayakutoa elimu ya Sekondari kwa viijana wengi,ni kituo cha Uinjilisti ambacho tangu mwaka 2007 kimebatiza watu 1,258 wengi kutoka Madhehebu mbalimbali.
Hata hivyo,amesema Shule ya Nyanza inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa mabweni kwawanafunzi wa kike nakiume,nahakunaJengo la Ibada na Mikutano.
Mwalimu Isaac Mwailafu ni mmoja kati ya Wazee watatu waKanisa la Shule hiyo ya Nyanza, ambayo ina wanafunzi wa Kidato cha Kwanza hadi cha Nne,ambayo iko eneo la Nyakato nje kidogo ya Jiji la Mwanza.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Sosthenes Maregesi Mugunda, ametoa wito kwa Jamii nzima kuichangia shule hiyo ili iweze kuimarishaTaaluma naMalezi,sambamba nakuwa kituo bora cha Uinjilisti jijini Mwanza.
PICHA/HABARI NA Kirumba sda Facebook Page
Baadhi ya waumini wa kanisa la Kirumba wakifatilia ibada hiyo hapo jana
Mwalimu Isaac Mwailafu ni mmoja kati ya Wazee watatu wa Kanisa la Shule ya Nyanza akisema jambo wakati wa hubiri siku ya Sabato hapo jana
Mwalimu Isaac Mwailafu ni mmoja kati ya Wazee watatu wa Kanisa la Shule ya Nyanza akisema jambo wakati wa hubiri siku ya Sabato hapo jana
Baadhi ya waumini wa kanisa la Kirumba wakifatilia ibada hiyo hapo jana
Baadhi ya waumini wa kanisa la Kirumba wakifatilia ibada hiyo hapo jana


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA