Hatimaye bajeti za nchi za Afrika Mashariki zimesomwa rasmi kufuatia utaratibu waliojiwekea kwa kusoma bajeti hizo katika siku moja iliyokubaliwa. Alhamisi ya tarehe 11 ya mwezi huu wa 6 ndiyo imekuwa siku ya kuweka wazi makadirio hayo ya mwaka 2015/16
![]() |
Tanzania |
![]() |
Kenya |
![]() |
Uganda |
![]() |
Rwanda |


Kupitia makadirio hayo ambayo yanategemewa kufanya maboresho na kufuta makosa yaliyoonekana nyuma, nchi zote hizi zimepunguza kodi za bidhaa zinaozoagizwa kutoka nje kwa sekta muhimu kama vile kawi,mawasiliano na miundo mbinu.
Kwa upande wa Nchi ya Rwanda, imepunguza kodi katika magari yanayoagizwa kutoka nje hususani matinga tinga,malori pamoja na mabasi ya uchukuzi.
Wakati Rwanda wakifanya hilo, majirani zao Tanzania nao kwa kiasi fulani wamelalia pia katika upande kama huo kwa kupunguza kodi ya
kuagiza bidhaa kutoka nje kutoka asilimia 25 hadi 10 miongoni mwa mabasi
yanayobeba abiria 25 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kenya na Uganda wao wametangaza kupunguza masharti kadhaa ya kibiashara kupitia kuondoa forodha ya
usalama katika uagizaji wa baadhi ya bidhaa ili kwa kiasi fulani kuleta uwiano.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment