Tuesday, June 02, 2015

Jumanne
Kumfuata Yesu katikaMaisha ya Kila Siku

 

Jiandae na Ukeshe

“Kukesha na uaminifu vinahitajika kwa wafuasi wa Kristo katika kila kipindi. Kwa kuwa sasa tupo katika ukingo wa ulimwengu wa milele, na tunaushikilia ukweli tulionao, na tuna nuru kuu ambayo ni kazi muhimu mno, sharti tuongeze bidii yetu.”—Ellen G. White, Testimonies for the Church,vol. 5, pp. 460, 461.

Soma Luka 12:35–53 na andika kwa ufupi kile ambacho aya hizi zamaanisha kwako, hasa ikiwa umekuwa ukisubiri kwa muda mrefu marejeo ya Yesu.







Kamwe Wakristo hawapaswi kuwa wazembe au kusinzia. Uhakika wa Kuja Kwake, na kutofahamika kwa saa ya kuja Kwake, vyahitajika vitufanye tufue mavazi yetu na kuzitengeneza taa zetu na kuhakikisha kuwa zinawaka. Sharti tumaini hili la siku za mwisho liwe ni motisha wa maisha na kazi yetu, utayari wetu na uaminifu wetu. Ni uaminifu huu wa kutenda mapenzi Yake duniani na utayari wa kukutana Naye kwa amani ndio hupambanua kati ya watumishi wema na waovu.

Kukosa uaminifu uwao wote ule kwa kuikiria na kusema kwamba “‘Bwana wangu anakawia kuja’” (Luka 12:45)humfanya mtu awe chini ya hukumu kali ya Mungu (aya 45–48).Kwa aliyepewa fursa kubwa, atahitajika kuwajibika zaidi, kwa hivyo, wale waliopewa vingi, wanatarajiwa watoe vingi (aya 48).

Hukumu ya nabii wa kale “Ole wao wanaostarehe katika Sayuni” (Amos 6:1)inaakisiwa katika onyo la Kristo kwamba uanafunzi wa Kikristo sio starehe. Paulo anaelezea maisha ya Kikristo kama vita vya kiroho(Efe. 6:12).La msingi ni kwamba kila Mkristo anajumuishwa katika pambano la Kiulimwengu kati ya Kristo na Shetani, na Msalaba unatupambanulia mambo hayo mawili kwa uwazi mno. Ni kwa imani ya kuendelea katika Kristo huyu wa msalaba ndio mtu anaweza kuupata ushindi wa mwisho.

“‘Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi’”(Luka 12:48). Aya hii yapasaimaanishe nini kwetu sisi kama Waadventista wa Sabato?



BOFYA HAPA SOMA LESSONI HAPA KILA SIKU NA 3angelsministry
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA