Thursday, June 04, 2015

Na Mwinjilisti Mwangosi
Nimepokea maswali mengi juu ya Sheria ya Vyakula, kama bado tunapaswa kuitii baada ya kuzaliwa mara ya Pili au Laa? Rejea fungu la maandiko - Wakolosai 2:16-17.
Kwa ufupi Sheria za Vyakula ziko za aina Mbili kubwa kama zifuatavyo:
1. Sheria za Vyakula kwa ajili ya AFYA, yaani chakula kisafi na kichafu (Visivyofaa kwa Afya). Mambo ya Walawi sura ya 11:1-47, Isaya 66: 16-17, pia Mwanzo 7:2 Mungu anatoa agizo juu ya wanyama Safi na Wasiosafi. Sheria hizi ni kwa ajili ya kulinda Afya za watoto wa Mungu.
- Mungu kama muumbaji wa miili yetu na muumbaji wa vyakula, anajua vyakula vipi vinafaa na vipi havifai kwa Afya zetu. Sheria hizo ni sawa na "Operations Manual" au maelezo yanayotolewa na mtengenezaji wa Gari au chombo chochote - ikionyesha namna ya kukitumia chombo. Magonjwa siku hizi ni mengi kwa sababu wanadamu wameamua kula na kunywa kila kitu. Ndio walevi wanaongezeka kila siku, wakidai neno linasema mtu na asiwahukumu.
Mungu anajali afya - 1Yohana 1:1-2, ukiharibu mwili (Hekalu) kwa kunywa na kula kila kitu - Naye Mungu atakuharibu - 1Wakorintho 3:16-17.
2. Sheria za Vyakula na Vinywaji kwa ajili ya Huduma maalumu ya Kafara au Upatanisho. Mambo ya walawi Sura ya 23:9-44. Sheria hizi ndizo zilikuwa kivuli cha Kifo cha Yesu msalabani, ambaye ndiye alikamilisha huduma ya Kafara. Vyakula na vinywaji vilitolewa Kwa ajili ya Sadaka maalumu vikitumika wakati wa huduma za upatanisho. Pia ziliambatana na sheria za Mapumziko (Sabato za siku za Upatanisho, Miezi, wiki, mwaka, mashamba), sheria zote hizi ziliisha baada ya kafara halisi kutolewa pale msalabani Kupitia kifo cha Yesu Kristo.
- Hizi ndizo Paulo aliwakataza Wakolosai wasihukumiwe na Wayahudi, walizokuwa wakilazimishwa kuzifanya baada ya Kifo na ufufuo wa kristo. Wakolosai 2:16-17.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA